Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Soma Biblia Kila Siku 4Mfano

Soma Biblia Kila Siku 4

SIKU 27 YA 30

Somo hili huthibitisha kwamba imetupasa kuingia katika ufalme wa Mungu kwa njia ya dhiki nyingi(Mdo 14:22), kwa kuwa kama wasioamini walivyomwudhi Yesu, wanawaudhi pia wamfuatao (m.14f). Lakini kwa sababu Injili ni Neno la Mungu (m.13), huwapa waumini kushinda dhiki hizo wapate kuokoka, bali wapinzani wake watapatwa na hasira ya Mungu (m.16; ling. 1:10 ilipoandikwa kuhusu Mwana wa Mungu:naye ni Yesu, mwenye kutuokoa na ghadhabu itakayokuja). Kazi yote ya Paulo hulenga kuja kwa Bwana wake Yesu (m.19). Furaha yake ni kumletea waumini wengi wanaomsifu. Je, ni furaha yako pia, ukifanya kazi ya Mungu?

siku 26siku 28

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 4

Soma Biblia Kila Siku 4 inakupa mpango wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu, hasa kutoka Kitabu cha Kutoka, na 1 Wathesalonike, pamoja na maelezo juu ya somo hilo.

Tungependa kushukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha