Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Soma Biblia Kila Siku 4Mfano

Soma Biblia Kila Siku 4

SIKU 26 YA 30

Injili huleta upinzani kwa sababu ni habari njema na wanadamu ni waovu. Lakini Injili humbadilisha mtumishi wake, kwa hiyo Paulo alikabili upinzani huo kwa moyo mweupe (m.5f), akifanya kazi yake kwa ujasiri (twalithubutu katika Mungu kuinena Injili ya Mungu kwenu; 2:2) pasipo na nia danganyifu (maonyo yetu siyo ya ukosefu, wala ya uchafu, wala ya hila; 2:3 na m.6), bila kutafuta fedha wala heshima (hatukuwa na maneno ya kujipendekeza wakati wo wote; kama mjuavyo, wala maneno ya juujuu ya kuficha choyo; rudia pia m.6), na bila kuchoka (m.9). Hivyo twafunga vinywa vya wapinzani! Tafakari pia jinsi Paulo alivyowapenda Wathesalonike kama watoto wake mwenyewe (m.7f na 11), kwa kuwa Mungu alikuwa amewaita wawe watoto wake (m.12).

siku 25siku 27

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 4

Soma Biblia Kila Siku 4 inakupa mpango wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu, hasa kutoka Kitabu cha Kutoka, na 1 Wathesalonike, pamoja na maelezo juu ya somo hilo.

Tungependa kushukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha