Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 4Mfano

Soma Biblia Kila Siku 4

SIKU 20 YA 30

Somo la leo lahusu mateso ya Yesu msalabani. Adui wengi walimsonga kama fahali wakali na simba walio tayari kurarua. Askari aligawanya nguo zake na vazi lake walilipigia kura (m.18; ling. Yn 19:23-24 ilipoandikwa: Askari walipomsulibisha Yesu, waliyatwaa mavazi yake, wakafanya mafungu manne, kwa kila askari fungu lake; na kanzu nayo. Basi kanzu ile haikushonwa, ilikuwa imefumwa yote pia tangu juu. Basi wakaambiana, Tusiipasue, lakini tuipigie kura, iwe ya nani. Ili litimie andiko lile linenalo, Waligawanya nguo zangu, Na vazi langu wakalipigia kura. Basi ndivyo walivyofanya wale askari). M.14-15 inaeleza kamili jinsi ajisikiavyo mtu aliyesubulishwa. Na tafsiri nyingine kwa "wamenizua" katika m.16 ni "wamenitoboa" (taz. Biblia Habari Njema). Yesu alipewa kovu za misumari mikononi na miguuni (ling. Tomaso na Yesu wanavyosema katika Yn 20:25 na 27: Mimi [Tomaso] nisipoziona mikononi mwake kovu za misumari, na kutia kidole changu katika mahali pa misumari, na kutia mkono wangu katika ubavu wake, mimi sisadiki hata kidogo. [Yesu]akamwambia Tomaso, Lete hapa kidole chako; uitazame mikono yangu; ulete na mkono wako uutie ubavuni mwangu, wala usiwe asiyeamini, bali aaminiye). Hata hivyo Yesu aliendelea kumtegemea Mungu kuwa nguvu zake zote (m.19).

siku 19siku 21

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 4

Soma Biblia Kila Siku 4 inakupa mpango wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu, hasa kutoka Kitabu cha Kutoka, na 1 Wathesalonike, pamoja na maelezo juu ya somo hilo.

More

Tungependa kushukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz