Soma Biblia Kila Siku 4Mfano
Mafundisho juu ya Chakula cha Bwana yanahitajika zaidi, kwa sababu sakramenti hii ni ya muhimu sana kwetu Wakristo. Jambo la msingi ni kwamba, tunaula mwili wa Kristo na kuinywa damu yake, yaani, twapokea matokeo ya kafara ya nafsi yake aliyoitoa ili kutupatia wokovu. Kwa hiyo ni muhimu sana kujihoji kabla ya kushiriki, kama kweli tunatafuta neema ya kukombolewa, kwa sababu bila kupokea kwa imani hatuwezi kukwepa hukumu (m.28-29). Hii ni sakramenti ya wokovu wetu, tusiichezee.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 4 inakupa mpango wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu, hasa kutoka Kitabu cha Kutoka, na 1 Wathesalonike, pamoja na maelezo juu ya somo hilo.
More
Tungependa kushukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz