Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Soma Biblia Kila Siku 4Mfano

Soma Biblia Kila Siku 4

SIKU 17 YA 30

"Eloi, Eloi, lama sabakthani?"Ndivyo Yesu alivyolia msalabani (Mt 27:46). Ni maneno ya kwanza ya somo la leo. Mwimba Zaburi alijisikia ameachwa na Mungu. Hata hivyo aliendelea kumtegemea. Hivyo ni mfano wa Yesu aliyesikia uchungu usiopimika wa kuachwa na Mungu alipobeba dhambi ya ulimwengu. Angalia kuwa wale waliomdhihaki Yesu walinukuu m.8. Maana katika Mt 27:43 imeandikwa: Amemtegemea Mungu; na amwokoe sasa, kama anamtaka; kwa maana alisema, Mimi ni Mwana wa Mungu. Mungu hakumponya Yesu, maana alitaka kuupatanisha ulimwengu na nafsi yake kwa njia ya kifo chake. Mungu asifiwe, maana awaokoa wote wamtumainiao.

siku 16siku 18

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 4

Soma Biblia Kila Siku 4 inakupa mpango wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu, hasa kutoka Kitabu cha Kutoka, na 1 Wathesalonike, pamoja na maelezo juu ya somo hilo.

Tungependa kushukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha