Hekima Kamilifu: Safari ya Siku 7 ya akina BabaMfano
Urithi wako kwa kizazi kinachokuja ni kipi?
"Kile baba anachofuata na nguvu, watoto wake watafuata kwa kiasi, kile baba anafuata kwa kiasi, watoto wake watapuuza...na hujui jinsi umefanya mpaka uone kile wajukuu wako wamefanta!"
Niliposkia mzungumzaji akisema hili, nilitetemeka. Haiwezi kuwa kweli, sio kila wakati. Lakini alitumia mifano mingi kutoka Andiko.
Ibrahimu. Mcha Mungu. Mtiifu. Aliunda nenoimani. Isaka kijana wake? Alikuwa mcha Mungu, lakini wakati mwingine alikiuka maagizo ya Mungu na kuelekea Misri. Na kulikua na wakati ule alipitisha bibi yake kama dada yake, dhambi ambalo lilifanana na la baba yake miaka iliyopita.
Nadharia ya mzungumzaji inasimama unapoangalia watoto wa watoto wao?
Watoto wa Isaka, Yakobo na Esau walikuwa wamcha Mungu. Lakini Yakobo alidanganya ili apate urithi wake, siyo? Na Esau aliibadilisha kwa haraka na bakuli la supu?
Cha muhimu ni kwamba sisi babalazimatumfuate Mungu kwanguvu, sio uhafifu. Watoto wetu wanaamua kwa ufasaha jinsi imani yao itakuwa muhimukwao kwa kuangalia jinsi imani yetu ni muhimu kwetu.
Usibahatishe. Jirushe ndani kabisa. Amua kuwa wazi, mcha Mungu, mwombaji, mtoa sadaka, mpenda Yesu, aliyejawa na neema za mfuasi wa Yesu.
Unaweza kujua, kuanzia siku hii kuenda mbele, kwamba ulimfuata Mungu na nguvu yako yote, Mtu yeyote asikuite vuguvugu tena.
Na labda wajukuu wako watakuwa na fursa na bahati!
Swali: Watoto wako watakueleza kama mwenye bidii katika mapenzi yako kwa Mungu?
Mpango huu umekuchangamsha kama baba?
Jifunze zaidi kuhusu Ibada ya Hekima Kali .
Kuhusu Mpango huu
Inashangaza kiasi ambacho baba zetu wanatufinyanga. Hakuna mtu anayeepuka nguvu na mvuto wa baba yao wa kidunia. Na kwa sababu wanaume wengi wanahisi kuwa hawako tayari kuwa baba, ni muhimu kutafuta mwongozo – kwenye Maandiko na kutoka kwa baba wengine. Hekima Kamilifu ni safari kuelekea hekima na busara kwa kina baba, inayohusisha kanuni na hekima kutoka kwenye Maandiko pamoja na uzoefu wa baba mwenye umri mkubwa na hekima zaidi ambaye amejifunza kutokana na makosa yake.
More