Hekima Kamilifu: Safari ya Siku 7 ya akina BabaMfano
Kondoo Bila Mchungaji
Watoto ni kama kondoo. Wako njia ya kuelekea uhuru, lakini kwa sasa, wanasukumwa na ujana na nguvu-na wanapitia hatari kwa sababu hawana uzoefu.
Kama kondoo, wanahitaji mchungaji.... mtu wa kuwaangalia. Wanahitaji baba. Baba halisi. Cha kusikitisha, najua watoto wengi wanakua bila mchungaji.
Natumaini kwamba wewe ni mmojawapo wa baba ambao wanachunga kwa makini. Baba ambaye ni mchungaji anafanya nini?
- Hutunza - Kama vile wachungaji wanajua kondoo walipo, baba wanajua watoto wao walipo.... kimwili, kimahusiano, na kiroho.
- Huchunga - Wachungaji huweka makundi yao pamoja. Baba wana jukumu kama hili, na huanza na kukaa na mke. Huwezi kuchunga kondoo wako wadogo pamoja kama kondoo wawili wakubwa hawakai pamoja.
- Hulisha - Wachungaji ndio wa kwanza kuwatafutia kondoo chakula. Baba wanatakiwa kuwafanyia watoto wao hivi pia. Baba hafai kutupa watoto wake.... haswa kama Mkristo. Zaidi ya kukimu mahitaji ya kimwili, Baba lazima wawape mapenzi yasiyo kifani watoto wao, pamoja na kukimu mahitaji ya kiroho.
- Hulinda - Wachungaji lazima wafanye chochote kinachotakiwa kufukuza mtu yeyote au kitu chochote kitakachoumiza kondoo wao au kuwapotosha. Baba hulinda watoto wao dhidi ya maumivu kutoka nje na kutowaumiza kupitia hasira, kutofikiria au kutojali.
Baba wengi watawacha kikundi chao cha kondoo tisini na tisa kwenda kumtafuta kondoo mmoja aliyepotea. Wewe pia utatunza, utachunga, utalisha na utalinda kondoo wako?
Swali:Wewe hutilia maanani kuangalia kama kondoo wako mmoja anapotea?
Kuhusu Mpango huu
Inashangaza kiasi ambacho baba zetu wanatufinyanga. Hakuna mtu anayeepuka nguvu na mvuto wa baba yao wa kidunia. Na kwa sababu wanaume wengi wanahisi kuwa hawako tayari kuwa baba, ni muhimu kutafuta mwongozo – kwenye Maandiko na kutoka kwa baba wengine. Hekima Kamilifu ni safari kuelekea hekima na busara kwa kina baba, inayohusisha kanuni na hekima kutoka kwenye Maandiko pamoja na uzoefu wa baba mwenye umri mkubwa na hekima zaidi ambaye amejifunza kutokana na makosa yake.
More