Hekima Kamilifu: Safari ya Siku 7 ya akina BabaMfano
Kuwa navyo vs. Kukosa
Kulea ni kugumu. Ni moja kati ya kazi ngumu. Hakuna kitabu cha mwongozo, hakuna kanuni ya kufuata, na Mungu anatutupia malezi na kumfanya kila mtoto tofauti. Kwa muda, unashika kanuni ambayo unaona inafaa; unaijaribu, na kama ikifanya kazi, inakuwa ya kwako.
Kwa hiyo nitapendekeza moja: tengenezaa mazingira ya kuwa navyo kwa watoto wako.
Watoto wanataka upendo. Kama kwa kila kitu duniani hapa, kinapokuwa pungufu, basi kinakuwa cha thamani sana na kuleta mashindano. Kama vipo tuu, siyo cha muhimu.
Chukua mafuta na chumvi kama mifano. Kila nchi inahitaji mafuta, kwa hiyo kuna ushindani mkali kwa ajili ya mafuta. Bei ni kubwa na kutarajia kupanda zaidi. Tunagombea, tunashawishi, tunahonga, tunauza nafsi zetu kwa ajili ya mafuta.
Kwa upande mwingine, chumvi ni muhimu kwa maisha ya binadamu, lakini ipo ya kutosha. Bei ya boksi la chumvi ni hela kidogo tuu. Ip nyingi.
Wakati akina baba wanaposhindwa kushikamana na watoto wao, wanapokuwa na shughuli nyingi watoto wao hawaoni kamawa muhimu, wakati uwepo wa baba ni mdogo nawala hana muda wa kuwa nao, hayo ni mazingira ya kuadimika.
Lakini akina baba wanapotoa upendo usio na mwisho, wakati upendo wao unapatikana wakati wote, kutakuwa na mashindano kidogo, kujipendekeza kidogo, na amani zaidi nyumbani. Baba inabidi awepo kimwili na kihisia.
Mazingira ya kupatikana hayaji kirahisi, na siyo rahisi.
Lakini ni bora zaidi.
Swali: Nyuma yako ni ya mazingira ya kuwepo au mazingira ya kupungukiwa? Watoto wanastawi katika mazingira ya kuwepo. Wanataabika katika mazingira ya kupungukiwa.
Kuhusu Mpango huu
Inashangaza kiasi ambacho baba zetu wanatufinyanga. Hakuna mtu anayeepuka nguvu na mvuto wa baba yao wa kidunia. Na kwa sababu wanaume wengi wanahisi kuwa hawako tayari kuwa baba, ni muhimu kutafuta mwongozo – kwenye Maandiko na kutoka kwa baba wengine. Hekima Kamilifu ni safari kuelekea hekima na busara kwa kina baba, inayohusisha kanuni na hekima kutoka kwenye Maandiko pamoja na uzoefu wa baba mwenye umri mkubwa na hekima zaidi ambaye amejifunza kutokana na makosa yake.
More