Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Hekima Kamilifu: Safari ya Siku 7 ya akina BabaMfano

Radical Wisdom: A 7-Day Journey For Fathers

SIKU 1 YA 7

Unapata Unachotukuza

Umewahi kutazama msichana mdogo “anapopodolewa” na mama yake, akiweka vipodozi, rangi ya mashavu, wanja, na rangi ya mdomo kwa mara ya kwanza akiwa bado ni mtoto? Kisha anamwambia jinsi ambavyo yeye ni mrembo, si kwa sababu yeye ni mrembo, bali ni kwa sababu yeye (ama mama yake) ametia juhudi.

Umewahi kutazama mchezo wa ligi ndogo na kuona baba akishangilia kwa furaha mwanaye akigonga mpira ama kufaulu? Wanapiga mikono hewani anapoteleza na kufunga bao.

Nimeishi muda mrefu na kuweza kuona watoto wengi wakikua na kuwa watu wazima, na nimekuja kuona kwamba unapata unachotukuza!

Tunapotumia wakati mwingi na pesa nyingi kuwavisha watoto na vijana wako ili wang'are, tutapata “farasi wa nguo” wanapokua. Ikiwa watoto wetu wa kiume wanatukuzwa kwa ufanisi wao katika michezo pekee, tutapata wachezaji wa kupita kiasi wakikua.

Hakuna makosa kwa nguo wala vipodozi, hakuna makosa kwenye michezo.

Lakini ujue ni nini unatukuza katika watoto wako.

Katika msamiati wangu, neno “tukuza” ni sawa na neno “sifa.” Watoto wako watafuata wenyewe wakikua unachosifu ndani yao.

Fikiria kutukuza wema wa mtoto wako kwa wengine. Uwakute wakifanyia ndugu zao vitu. Uwasifu kwa hayo. Uwatukuze kwa kuomba, kusoma Biblia, kuuliza kuhusu Yesu, na kutoa pesa kanisani, shirika la hisani, ama maskini.

Kumbuka, siku zote unaongoza. Swali ni kuelekea wapi.

Swali: Utaongoza kwa kutukuza unachotumaini kupata watoto wako wanapokua kuwa watu wazima?

siku 2

Kuhusu Mpango huu

Radical Wisdom: A 7-Day Journey For Fathers

Inashangaza kiasi ambacho baba zetu wanatufinyanga. Hakuna mtu anayeepuka nguvu na mvuto wa baba yao wa kidunia. Na kwa sababu wanaume wengi wanahisi kuwa hawako tayari kuwa baba, ni muhimu kutafuta mwongozo – kwenye Maandiko na kutoka kwa baba wengine. Hekima Kamilifu ni safari kuelekea hekima na busara kwa kina baba, inayohusisha kanuni na hekima kutoka kwenye Maandiko pamoja na uzoefu wa baba mwenye umri mkubwa na hekima zaidi ambaye amejifunza kutokana na makosa yake.

More

Tungependa kuwashukuru Radical Mentoring kwa kutoa mpango huu. Kwa maelezo zaidi, tembelea tuvuti: http://radicalwisdombook.com