Hekima Kamilifu: Safari ya Siku 7 ya akina BabaMfano
Chakula cha jioni Pamoja
Naweza kuhesabu vitu mke wangu amekuwaanasisitiza peke yake. Chakula cha jioni ni mojawapo.
“Utarudi saa ngapi?” alikuwa anauliza. “Nimetingwa . . . nitachelewa kidogo” namwambia. Hakushtuka, atageuza, “Jifungue na uingie barabarani. Tuna chakula cha jioni cha pamoja katika familia hii.Kitakuwa tayari na kitakuwa mezani saa 12.30!”
Ninaongeze chumvi kidogo, lakini siyo sana. Mke wangu siku zote alisisitiza kula chakula cha jioni pamoja kama familia. Mara ya kwanza haikuonekana kama ni muhimu sana.
Lakini kadri muda ulivyokwenda, na watoto wangu kuingia ujanani, niliona thamani yake. Ilikuwa ni muda huo kila siku ambapo tulitazamana usoni. Tulizungumza mambo. Tuliweza kusikia mioyo yao ikidunda na wao kusikia yetu.Waliweza kuona jinsi wazazi wao walivyozungumza, walivyofanya kazi pamoja, na kupendana. Kaka na dada walikaa kwa tiba ndogo ya familia.
Kama siyo nyumbani, ni wapi watoto wako watajifunza juu ya upendo, kanuni za familia, utii, huruma, utatuzi wa matatizo, na msamaha? Nani atawaanda kwa ajili ya ndoa na maisha ya familia? Siijui "shule ya waume" au "shule ya wake" ambapo watoto wetu watasoma vitu hivi.
Swali: Je, familia yako inakaa pamoja nyumbani mara kwa mara? Jiulize mwenyewe, “Miaka ishirini kutoka sasa, wanavyopata kwenye shughuli za nje vitakuwa vya muhimu zaidi kuliko familia mnapokuwa moja na moja?”
Kuhusu Mpango huu
Inashangaza kiasi ambacho baba zetu wanatufinyanga. Hakuna mtu anayeepuka nguvu na mvuto wa baba yao wa kidunia. Na kwa sababu wanaume wengi wanahisi kuwa hawako tayari kuwa baba, ni muhimu kutafuta mwongozo – kwenye Maandiko na kutoka kwa baba wengine. Hekima Kamilifu ni safari kuelekea hekima na busara kwa kina baba, inayohusisha kanuni na hekima kutoka kwenye Maandiko pamoja na uzoefu wa baba mwenye umri mkubwa na hekima zaidi ambaye amejifunza kutokana na makosa yake.
More