Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Hekima Kamilifu: Safari ya Siku 7 ya akina BabaMfano

Radical Wisdom: A 7-Day Journey For Fathers

SIKU 6 YA 7

Baba wanaofuata Yesu Kristo 

Baba wanaofuata Yesu huanza kwa kusaidia watoto wao kuelewawao ni nani kwa Mungu. Mtoto wako anajua kwamba yeye ni mtoto aliyeasiliwa na Mfalme wa Wafalme-amesamehewa kabisa, anatosha kabisa na ana thamani kamili?

Watoto wakianza kuelewa wao ni nani kwa Mungu, wanagundua utambulisho ulio na maana. Utambulisho huo hufanya kuwa rahisi kujua utakachofanya nyakati ambazo uzuri na ubaya hautambuliki kwa urahisi, au wazazi wanapobishana na uamuzi wao.

Mchakato wao wa uamuzi hugeuka kuwa "Yesu angetaka nifanye nini?" kwa sababu uhusiano wao na Yesu ni msingi wa utu wao.

Marafiki wangu Craig na Kerry wana binti watatu wa ajabu. Uamuzi kati ya sketi au blauzi fupi unapotokea, Kerry huuliza "Unadhani kwamba inafaaa?" Watoto wengi wangebishana, wakifikiria mama anawawekea fikira za kinachofaa kwao.

Lakini wasichana hawa wamejitengenezea utambulisho wao.... viwango vyao vya kinachofaa na kisichofaa. Wameepuka vita kuhusu kinachoweza kuvaliwa au la kwa sababu wamejiamulia. "Najua mimi ni nani. Watu kama mimi hawavai nguo kama hizo. Watu kama mimi hawafanyi vitu hivyo."

Swali: Utalenga kujitambulisha kwa watoto wako, ili uwaongoze wajue wao ni nani katika Yesu?

siku 5siku 7

Kuhusu Mpango huu

Radical Wisdom: A 7-Day Journey For Fathers

Inashangaza kiasi ambacho baba zetu wanatufinyanga. Hakuna mtu anayeepuka nguvu na mvuto wa baba yao wa kidunia. Na kwa sababu wanaume wengi wanahisi kuwa hawako tayari kuwa baba, ni muhimu kutafuta mwongozo – kwenye Maandiko na kutoka kwa baba wengine. Hekima Kamilifu ni safari kuelekea hekima na busara kwa kina baba, inayohusisha kanuni na hekima kutoka kwenye Maandiko pamoja na uzoefu wa baba mwenye umri mkubwa na hekima zaidi ambaye amejifunza kutokana na makosa yake.

More

Tungependa kuwashukuru Radical Mentoring kwa kutoa mpango huu. Kwa maelezo zaidi, tembelea tuvuti: http://radicalwisdombook.com