Hekima Kamilifu: Safari ya Siku 7 ya akina BabaMfano
Baba mwenye masikitiko machache
Kulikua na wakati katika biashara ambapo "njia ya busara" kwenye maamuzi ilitawala. Tulitengeneza fomula na kubashiri welekeo wa juu iwezekanavyo wa kufaulu na wa chini iwezekanavyo wa kutofaulu. Tulicheza na uwezekano wa kufaulu au kushindwa kwamba tukifanya mambo fulani, nyakati nyingi tutashinda.
Kama baba, hatutaki "kucheza na uwezekano wa kushindwa au kufaulu" na watoto wetu. Hata kama iweje, hatuwezi hakikisha kwamba watatokea wakiwa wazuri zaidi, wakifuata mwelekeo wa Yesu Kristo. Lakini tunaweza kufanya maamuzi ambayo yatasabibisha masikitiko madogo sana kwetu! Tunaweza kuchagua mambo ambayo hatutajuta baadaye.
Wanaume wengi wanaishi na maamivu mengi kutoka kwaa baba zao ambao hawakudhibiti ndimi na hasira zao. "Baba, usikasirishe watoto wako; badala yake, walee kwa mafunzo na mwelekeo wa Mungu" Kwa kadri iwekzekanavyo, lazima tunyamaze. Dhibiti ukosoaji na hasira zetu. Mara nyingi hatuwezi kuona kama tunaifanya..... mpaka imefanyika.
Tulitamani kusikia maneno ya kusifu na kuthibitisha kutoka kwa Baba zetu, lakini wengi wetu hatukuyasikia. Ni maajabu jinsi kiburi kinavyotulemaza. Tutasafiri na magari ya ng'ombe na pikipiki, lakini hatuwezi kupita hofu zetu za tutaonekanaje au kwa taratibu tukiwaambia wasichana na wavulana wetu jinsi wao ni maalum na jinsi gani tunawapenda.
Wote mtasimamia watoto wenu? Unalea ili baadaye uje kuwa na majuto kidogo kama baba miaka mingi kuanzia sasa?
Swali: Utamwuliza Mungu akuoneshe ni nini utakachofanya ambacho utajuta zaidi kama baba miaka kadhaa ijayo? Kisha umwulize akupe ujasiri kusahihisha?
Kuhusu Mpango huu
Inashangaza kiasi ambacho baba zetu wanatufinyanga. Hakuna mtu anayeepuka nguvu na mvuto wa baba yao wa kidunia. Na kwa sababu wanaume wengi wanahisi kuwa hawako tayari kuwa baba, ni muhimu kutafuta mwongozo – kwenye Maandiko na kutoka kwa baba wengine. Hekima Kamilifu ni safari kuelekea hekima na busara kwa kina baba, inayohusisha kanuni na hekima kutoka kwenye Maandiko pamoja na uzoefu wa baba mwenye umri mkubwa na hekima zaidi ambaye amejifunza kutokana na makosa yake.
More