Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

MUNGU + MALENGO: Jinsi Ya Kuweka Malengo Kama MkristoMfano

GOD + GOALS: How To Set Goals As A Christian

SIKU 4 YA 5

SIKU YA 4: Ninafanyaje malengo yangu kutimia na siyo kwenda nje ya mapenzi ya Mungu? 

Umesimama katika mstari wa kuanzia, unataka kufuata malengo yanayoongozwa na Mungu, na...unaogopa. Unaogopa kuchukua hatua kwenye malengo hayo, ukidhamiria kuyatimiza na kumwacha Mungu katika huo mchakato. Unawezaje kuweka mtazamo wako katika Mungu na kutimiza malengo yako wakati huohuo?

Kwanza kabisa, malengo sahihi yatakuongoza katika njia zake, si mbali na Yeye. 

Pili, hutaweza kuweka lengo na kutoka kwenye lengo. Mungu anataka ubaki umeunganishwa naye katika kila hatua, na atakuongoza. Mwishowe, yeye ndiyo lengo. Kufuata kusudi alilonalo kwa ajili yetu ni kama kufuata ramani aliyoitayarisha. Anaijua njia.

Kama ambavyo ungefanya kwenye safari ndefu, endelea kuangalia ramani kuwa na uhakika unaelekea sehemu sahihi. Kama ukipotea kwenye mpango wako, unaweza kujikuta uko kwenye mtaa usioufahamu. Lakini, anza tena, utarudi kwenye njia sahihi! Mungu hajali kama unafanikiwa au hufanikiwi katika lengo lako; anataka moyo wako. Hatua kwa hatua, maombi kwa maombi, muda kwa muda unapomtafuta, utabaki kwenye njia sahihi. Muunganiko naye utakufanya uwe katika uangalizi wake.

Omba nami: Bwana, ninaogopa kufuata njia ambayo siyo ya kwako. Naomba usinipe roho ya uoga, bali ya nguvu, upendo, na kiasi (2 Timotheo 1:7). Asante kwa ramani--dunia yako---na kwa uwezo wa kuomba moja kwa moja kwako! Nisaidie kuweka mtazamo kwako kama lengo langu badala ya kibali cha watu, marafiki, au fahari ya kuondoa vitu vya muhimu. Nataka kuwa na bidii kwako kwa sababu sahihi. Asante kwa kuniongoza na kunitunza katika njia yako! Katika jina la Yesu. Amen

siku 3siku 5

Kuhusu Mpango huu

GOD + GOALS: How To Set Goals As A Christian

Ni vyema kuweka malengo kama Mkristo. Unajuaje kama lengo lako ni kutoka kwa Mungu au kwako mwenyewe?. Na malengo ya kikristo yanaonekanaje? Katika siku 5 za mpango huu wa kusoma, utajifunza katika neno na kupata ufasaha na muelekeo juu ya kupanga mipango inayosukumwa na neema!

More

Tunapenda kuwashukuru Cultivate What Matters kwa kutoa mpango huu. Kwa taarifa zaidi, tafadhali tembelea: http://www.cultivatewhatmatters.com/youversion