Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

MUNGU + MALENGO: Jinsi Ya Kuweka Malengo Kama MkristoMfano

GOD + GOALS: How To Set Goals As A Christian

SIKU 1 YA 5

SIKU 1:  Ni vyema kuweka malengo kama Mkristo?

Unataka kumfuata Mungu NA kufikia malengo kwa kusudi. Lakini unamashaka kwamba kuweka malengo kutakuongoza mbali na mipango ya Mungu kwa ajili yako. Unajiuliza, " Ni sahihi kuweka malengo kama Mkristo? Neno la Mungu linasemaje kuhusu jinsi ya kufanya hili na kubaki katika mapenzi yake? Mungu ana mengi ya kusema kuhusu malengo, mipango ya makusudi, na kulinda vyema vile tulivyopewa.

Jibu fupi: malengo ni mazuri! Hata Yesu alikuwa na malengo. Mungu ana matumaini kwetu kuishi kwa kusudi, siyo kwa bahati mbaya. Kitendo cha kumwomba na kutafuta mapenzi yake maana yake unataka kuishi maisha haya vyema. Neno lake litakuangazia jinsi ya kupanga malengo sahihi na kushawishika kuyafikia. 

Lakini, usitarajie kuona orodha ya nini kifanyike au fomula ya namna ya kuweka malengo katika Biblia. Ingekuwa rahisi kiasi hicho, tungesoma orodha na kuchagua tunavyotaka, na tusizungumze na Mungu kuhusu mipango yetu. Siyo suala la kufuata kanuni, ni kuhusu uhusiano na Mmoja aliyekuumba na karama tofauti na vipaji kuvitumia, Mungu mwenyewe.  

Mbadala wa kuweka malengo mazuri? Kuzunguka bila lengo maalum, na maisha yaendelee. Fikiria juu ya hilo. Kuna yeyote katika watu maarufu katika Biblia alikaa tuu na kutokufanya chochote? Hakika, walikosea hatua wakati mwingine, lakini Musa, Daudi, Sulemani, Esta, Ruthu, Yohana, Paulo, na Yesu mwenyewe walikuwa na malengo, na waliyafikia kwa nguvu za Mungu na hekima. Karibia utafanya vivyo hivyo, hatua moja ndogo na ya imani kwa wakati.

Omba nami: Bwana, ninataka kukufuata, kupanga malengo yanayoendana na mapenzi yako kwa maisha yangu. Asante kwa kuniumba na karama na vipawa tofauti kuvitumia kwa kusudi kubwa. Ninataka kwenda unakokwenda. Tafadhali nionyeshe namna ya kuweka malengo jinsi unavyopenda. Ninahitaji hekima yako katika kupanga na kusudi ili niweze kuongoza kile ulichonipa-- muda wangu, fedha zangu, kazi yangu, mahusiano yangu, afya yangu-- mahali nilipo. Fungua macho yangu kwenye kweli yako na uisaidie kuhama kutoka kichwani mpaka moyoni na mikononi mwangu. Katika jina la Yesu. Amen!

siku 2

Kuhusu Mpango huu

GOD + GOALS: How To Set Goals As A Christian

Ni vyema kuweka malengo kama Mkristo. Unajuaje kama lengo lako ni kutoka kwa Mungu au kwako mwenyewe?. Na malengo ya kikristo yanaonekanaje? Katika siku 5 za mpango huu wa kusoma, utajifunza katika neno na kupata ufasaha na muelekeo juu ya kupanga mipango inayosukumwa na neema!

More

Tunapenda kuwashukuru Cultivate What Matters kwa kutoa mpango huu. Kwa taarifa zaidi, tafadhali tembelea: http://www.cultivatewhatmatters.com/youversion