Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

MUNGU + MALENGO: Jinsi Ya Kuweka Malengo Kama MkristoMfano

GOD + GOALS: How To Set Goals As A Christian

SIKU 3 YA 5

SIKU YA 3: Malengo yanayosukumwa na imani yanaonekanaje?

Malengo yanayoongozwa na Mungu yakoje? Unaweza kuwa na lengo ambalo waziwazi halina uhusiano na huduma-- kama kwenda tena shule? Au, malengo yako yote lazima yawe " omba zaidi", "nenda safari ya umisheni"na " tumika kanisani kwangu"?

Baadhi ya malengo na matendo tayari yameelezwa katika maandiko, ambayo hutusaidia: soma Biblia yako ( Zaburi 119:9), omba sana ( 1Wathesalonike 5:17-18), kuwa na waamini wengine ( Waebrania 10:25), na shiriki imani yako ( Zaburi 96:3). Mungu anapenda vitu hivi kutuweka karibu naye--kutufanya tuzae matunda na kuwa waaminifu. Hii siyo orodha ya kufuata, bali ni matokeo ya moyo uliobadirishwa kwa neema ya Mungu. Tunalazimika kufanya vitu hivi kwa sababu anatupenda sana.

Lakini maisha mengine je? Mungu anataka tufanye vitu vyote kwa utukufu wake ( 1 Wakorintho 12: 31)--malengo makubwa aliyonayo kwa ajili yetu na yanayoonekana ya kawaida. Ikiwa ni kuanzisha biashara, kumaliza shahada, kulea watoto, kufanya maamuzi mazuri ya kifedha, kuangalia mwili wako, au kuacha mbali kufua ( kufua kiroho? Ndiyo!),ikiwa vitu vyote hivyo vinafanyika kwa lengo la kumpendeza Mungu, unaweza kuvitumia kuwa mwanga kwa ajili yake. Haimaanishi tunatakiwa kuwa wakamilifu katika tabia zetu katika vitu vyote hivyo au maendeleo yetu, tunatakiwa kuwa waaminifu!  

Tunapofanya vitu vyote kwa utukufu wake, watu wanaona kitu cha tofauti ndani yetu. Wanashangaa tumaini letu linatoka wapi na, Bwana akipenda, tutapata nafasi ya kushiriki Chanzo. Kwa hiyo, malengo yako yoye yanatakiwa yawe kuhusu umisioni na kutumikia kanisa lako? Mahali popote Bwana amekuweka, stawi ulipopandwa. Piga mluzi wakati unafanya kazi, na hata kitu cha kawaida kinakuwa na maana!

Omba nami: Baba, asante kwa kunipanda mahali nilipo. Nisaidie kuchukua hatua juu ya mambo uliyoyaweka mbele yangu kwa macho ya kiroho, nikiyaona kama malengo ya kimungu, pasipokujali majukumu yangu. Nisaidie kila nachokifanya kukuonyesha wewe-- hata ninapokosea na kupungukiwa. Neema yako ikawe bendera yangu ninaposonga mbele kwenye malengo, nikijua si juu ya ukamilifu, bali Wewe-- mwanzilishi na mkamilishaji wa imani yangu. Katika jina la Yesu. Amen!

siku 2siku 4

Kuhusu Mpango huu

GOD + GOALS: How To Set Goals As A Christian

Ni vyema kuweka malengo kama Mkristo. Unajuaje kama lengo lako ni kutoka kwa Mungu au kwako mwenyewe?. Na malengo ya kikristo yanaonekanaje? Katika siku 5 za mpango huu wa kusoma, utajifunza katika neno na kupata ufasaha na muelekeo juu ya kupanga mipango inayosukumwa na neema!

More

Tunapenda kuwashukuru Cultivate What Matters kwa kutoa mpango huu. Kwa taarifa zaidi, tafadhali tembelea: http://www.cultivatewhatmatters.com/youversion