MUNGU + MALENGO: Jinsi Ya Kuweka Malengo Kama MkristoMfano
SIKU 2: Unajuaje kama lengo linatoka kwa Mungu au kwako mwenyewe?
Unaanza kuiona: pasipo malengo, unaweza kuzunguka pasipo kukusudia katika maisha. Malengo yanayoongozwa na Mungu ni mazuri. Lakini! Unajuaje kama yanaongozwa na Mungu na siyo kutoka kwako? Unawezaje kuyatofautisha? Unaogopa utachagua malengo yasiyo sahihi!
Je unajua ni kitu gani cha ajabu sana kuhusu Mungu? Mambo ni mengi, lakini kwa kuyataja, Anataka kufanya maisha haya sambamba na wewe. Unapojisikia umepotea katika malengo yako na kusudi, au katika kuchagua njia moja na nyingine, anataka umwombe akusaidie--na anapenda kutoa! Yakobo anatuambia, '“Lakini mtu wa kwenu akipungukiwa na hekima, na aombe dua kwa Mungu, awapaye wote, kwa ukarimu, wala hakemei; naye atapewa.” (Yakobo 1:5 SUV).
Hujui kama mipango yako ni mizuri kwa lengo?
Fanya uchunguzi kidogo:
- Fungua neno na tafuta maandako husika au habari katika Biblia inayothibitisha lengo ulilonalo kichwani. Je lengo lako liko sahihi kibiblia? Je, kuna maandiko yanayothibitisha hilo? “Kila andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki;” (2 TIM. 3:16 SUV).
- Mwombe! Mwombe Mungu akuonyeshe njia anayotaka uende. “Nitakufundisha na kukuonyesha njia utakayoiendea; Nitakushauri, jicho langu likikutazama.” (ZAB. 32:8 SUV)
- Waulize marafiki unaowaamini au washauri wanaompenda Mungu kwa muongozo. '“Pasipo mashauri makusudi hubatilika; Bali kwa wingi wa washauri huthibithika.” (MIT. 15:22 SUV).
Kumbuka, hakuna fomula inayoweza kufunua malengo yote isipokuwa Mungu mwenyewe. Kama jibu bado halionekani wazi, usikate tamaa! Hii inaweza kuwa sehemu ya mchakato anaotaka uupitie. Katika kungoja, tunasafishwa na kutayarishwa kwa hatua inayofuata. Subiri katika hekima yake, na atakupatia katika wakati wake sahihi!
Omba nami: Bwana, asante kwa neno lako! Ninakushukuru kwa miongozo yako na hekima. Tafadhali nisaidie kupambanua tofauti kati ya malengo na mipango itokanayo na upendo wangu kwako na mingine yote. Nisaidie kujua sauti yako, kuamini uongozi wako, na kukutafuta wewe zaidi ya kila kitu kingine. Katika jina la Yesu. Amen!
Kuhusu Mpango huu
Ni vyema kuweka malengo kama Mkristo. Unajuaje kama lengo lako ni kutoka kwa Mungu au kwako mwenyewe?. Na malengo ya kikristo yanaonekanaje? Katika siku 5 za mpango huu wa kusoma, utajifunza katika neno na kupata ufasaha na muelekeo juu ya kupanga mipango inayosukumwa na neema!
More