MUNGU + MALENGO: Jinsi Ya Kuweka Malengo Kama MkristoMfano
SIKU YA 5: Itakuwaje kama sitaweza?
Una malengo mazuri akilini mwako, na unaamini kwamba Bwana atakuongoza. Lakini, ukishindwa itakuwaje? Unaogopa hutaweza, utaharibu, na utamkatisha tamaa Mungu.
Kuna msemo maarufu unaosema, " Aliamini anaweza hivyo aliweza." Neno la Mungu linatufunulia, ukweli wa kutuweka huru: Aliamini hataweza, lakini Mungu aliweza. Hutakiwi ufanye mwenyewe, rafiki yangu. Mungu hatarajii uwe mkamilifu. Ndiyo maana alimtuma Yesu kuja kutuokoa--alijua tunahitaji mwokozi kuwa nguvu yetu tunapokuwa wadhaifu, kutuongoza, kutuonyesha njia, na kuondoa hukumu ya dhambi zetu. Injili ndiyo inachochea malengo yanayoongozwa na Mungu, kutusaidia kuhamasishwa kurudi kwenye njia tunapoanguka. Unakuwa hauwezi, Yeye anaweza. Na ukweli, tayari aliweza msalabani. Haijalishi unafanikiwa au hufanikiwi chochote, Mungu amekwisha kushinda mauti kwa ajili yako na mimi! Hakuna uharibifu ulioufanya ambao hawezi kuurekebisha na kuwa kitu kizuri.
Hebu na tuweke pamoja:
- Tafuta hekima yake kwenye malengo na mipango inayoongozwa na Mungu. Yeye atakupa!
- Chukua hatua za imani, katika malengo makubwa na inayoonekana kuwa na hatua ngumu katikati.
- Na mwamini katika kukumwagia neema yake Kwako katika mara nyingi utakazokosea-- kwa sababu utakosea tuu! Kama malengo yako yameelekezwa kwake, hutaacha. Utamgeukia kwa ajili ya nguvu na hekima, ukijua jinsi unavyoyafikia malengo haijalishi sana kuliko Sababu.
Omba na mimi: Bwana, imekuwa ni safari ya jinsi gani katika neno lako la uzima! Nisaidie kufanya kitu kutokana na nilichojifunza na zaidi ya yote, nisaidie kutangaza habari njema za Yesu. Malengo yangu yote, makubwa na madogo, yaniongoze miguuni pako. Na ninapokosea, nikumbushe juu ya neema inayobadirisha. Neema inisukume mbele kuishi katika kusudi lako la maisha yangu! Katika jina la Yesu. Amen!
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Ni vyema kuweka malengo kama Mkristo. Unajuaje kama lengo lako ni kutoka kwa Mungu au kwako mwenyewe?. Na malengo ya kikristo yanaonekanaje? Katika siku 5 za mpango huu wa kusoma, utajifunza katika neno na kupata ufasaha na muelekeo juu ya kupanga mipango inayosukumwa na neema!
More