Nenda Tenda Sema Toa: Uhuru wa Kujisalimisha kwa YesuMfano
Nitasema Unachohitaji Niseme
Smokey Bear amenikumbusha kwa zaidi ya miaka sabini kuwa "ni wewe tu unaeweza kuzuia moto wa misitu." Hasara ya hata cheche ndogo inaweza kuharibu msitu mzuri na kuharibu jamii nzima. Maandiko yanatumia msamiati huo huo kuelezea uwezo wa uharibifu wa maneno yetu: "Vivyo hivyo ulimi nao ni kiungo kidogo, nao hujivuna majivuno makuu. Angalieni jinsi moto mdogo uwashavyo msitu mkubwa sana!" (Yakobo 3:5)
Pamoja na uwezo wa uharibifu huo na pia uwezo wa mema ambao unakuja na usemi, ni muhimu kusema Yesu anachopenda tuseme, na sio tu kuiga maadili ya utamaduni wetu. Dunia imejazwa na semi zenye tabia ya chuki, wivu, hukumu na hasira. Yesu alitoa kanuni kuwa "kwenye wingi wa moyo mdomo huongea." Hatuwezi kukwepa ukweli; usemi wetu utaonyesha kilichopo ndani yetu"
Ni vipi kumfuata Yesu kuna athiri tunachokisema na kwanini. Ameelezewa kama "Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu" (Yohana 1:14). Yeye ndio mawasiliano ya mwisho ya Mungu kwa uumbaji wake. Na tuna ambiwa "neema na ukweli ulikuja kupitia Yesu Kristo." Anavyoishi ndani yetu, tutarajie kuzungumza na neema na ukweli. Maisha ya Yesu hayakuonyeshwa kwa upendo na maneno ya neema lakini kwa maneno ya uaminifu ambayo yali tafakari ukweli kuhusu yeye na dunia inayomzunguka.
Kwenye Matendo ya Mitume 1:8, Yesu aliwaambia wanafunzi wake kuwa Roho Mtakatifu atakapokuja juu yao na watapokea nguvu na kuwa mashahidi wake. Tunavyonyenyekea kwenye utawala wake, tutajikuta kwamba tunataka kuwaambia wengine kuhusu yeye. Hii haimaanishi hatukubaliani kwa wengine, kama wengine wenye hofu. Ki ukweli, ni kinyume: tutakuwa wema na wenye huruma, kuwaambia watu Yesu ni nani na mabadiliko aliyoyafanya kwenye maisha yetu.
Lakini kusema Mungu anachopenda tuseme haihusu tu kuwaambia watu kuhusu Yesu. Ni kutumia maneno yetu kuongea na wengine jinsi ambavyo Yesu angefanya: kuonyesha ukarimu na msamaha na kuthibitisha kwa wengine jinsi walivyo na vitu wanavyofanya vyema. Kwa kufanya hivyo, tunawabariki na kuwahamasisha katika safari ya kiroho.
Je kuna mabadiliko ya jinsi unavyotakiwa kuongea na mtu maishani mwako?Fikiria hata mtu mmoja jinsi utakavyo ongea tofauti kwake mara nyingine utakapo kutana naye
Utasema kile Mungu anataka useme leo?
Kuhusu Mpango huu
Kujisalimisha kwa Yesu ni tukio kubwa maishani. Lakini uamuzi huu unamaanisha nini na tutauishi vipi kila siku? Uamuzi ni wa mambo makubwa ya maisha pekee, ama wacha Mungu kupita kiasi? Woga, makosa yaliyopita, na kutoelewa vinaweza kutuzuia. "Nenda Tenda Sema Toa" ni ahadi/sala ambayo inafunua jinsi utakavyochukua hatua zinazofuata katika safari yako ya kiroho. Pata uhuru unaotokana na kumfuata Yesu.
More