Nenda Tenda Sema Toa: Uhuru wa Kujisalimisha kwa YesuMfano
Nitakwenda unapotaka niende.
Hakuna anayependa kukwama. Tuazungumza kuhusu kukwama katika desturi au kukwama kihisia kama kitu kibaya. Kukwama maana yake hakuna kwenda mbele au hakuna kukua. Na kiroho pia inatokea. Hebu tuwe wakweli, wote tunakubali mwamba huwa tunajisikia kama tumekwama katika safari yetu ya kiroho mara kwa mara. Habari njema ni kwamba Yesu yuko kwenye hatua ya kutupeleka mahali; kumfuata ni kusudi la maana ili tufike anapotaka tuwe, na atatufanya tusikwame muda mrefu kama tutamsikiliza.
Hiki ndicho Abram alifanya katika Mwanzo 12. Akiwa amekwamba katika mji wa kwao, Mungu anamwamuru Abram kuendelea na safari, akiachana na nchi yake na jamaa yake kwenda kwenye kwenye nchi Mungu atakayomwonesha. Matokeo ya hatua ya imani ya Abram itakuwa ni taifa jipya linalomheshimu Mungu na kupelekea kumleta Masihi kwa ukombozi wa wanadamu.
Waebrania 11: 8 inatuambia kwamba Abram alimtii Mungu na " kutoka, pasipo kujua anakwenda wapi". Akituonesha kwamba kwenda Mungu anakotaka uende mwishowe ni suala la imani- kutegemea katika wema na mpango kamili wa Mungu katika maisha yetu. Kunapotakiwa imani, siku zote ni hatari na wakati mwingine kuna hofu, kwa sababu hatujui yatakayotukabili. Kuchagua kwenda ni kuchagua kukabiliana na vyote hivyo.
Akiwa amemaliza kusudi lake duniani, Yesu aliwaagiza wanafunzi wake: " enendeni, na mkawafanye wanafunzi mataifa yote..." ( Mat. 28: 19). Katika maombi yake katika Yohana 17, anamwambia baba " kama ulivyonituma ulimweguni, nami nawatuma hawa ulimwenguni." Kwenda Yesu anakotaka twende kutatufanya kufanya wanafunzi," wafuasi wenzetu wa Yesu." Bahati mbaya, wengi wanachukulia agizo la "kufanya wanafunzi" kuwa ni kwa karama maalum, au maelezo ya taaluma fulani katika huduma. Lakini kuna njia nyingi za kushiriki katika kufanya wanafunzi.
Ni kazi ya kila mfuasi wa Yesu, kama ukarimu au maombezi. Unaponyenyekea kwa Roho ili aongoze maisha yako, mwambie Yesu utakwenda mahali atakapokwambia uende katika safari yako ya kiroho, ikiwemo kufanya wanafunzi. Mwache akuongoze jinsi ya kuwa na kuishi kila siku.
Utakwenda Mungu anapotaka niende leo?
Muombe nani unaweza kumshawishi leo kuwa mwanafunzi mwenzako wa Yesu.
Kuhusu Mpango huu
Kujisalimisha kwa Yesu ni tukio kubwa maishani. Lakini uamuzi huu unamaanisha nini na tutauishi vipi kila siku? Uamuzi ni wa mambo makubwa ya maisha pekee, ama wacha Mungu kupita kiasi? Woga, makosa yaliyopita, na kutoelewa vinaweza kutuzuia. "Nenda Tenda Sema Toa" ni ahadi/sala ambayo inafunua jinsi utakavyochukua hatua zinazofuata katika safari yako ya kiroho. Pata uhuru unaotokana na kumfuata Yesu.
More
Tungependa kushukuru Cru kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.cru.org/us/en/pledge.html