Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Nenda Tenda Sema Toa: Uhuru wa Kujisalimisha kwa YesuMfano

Go Do Say Give: The Freedom Of Surrender To Jesus

SIKU 7 YA 7

Kwa heshima na utukufu wako.

Kusalimisha maisha yetu kwa Yesu siyo kiapo cha ukamilifu; ni tamko la utii. Siyo jambo la mara moja katika maisha yetu. Ni kuanza upya na kulinganisha mioyo yetu na kuweka mawazo, hisia zetu na mapenzi yetu kujitoa kila siku kwenye mpango na kusudi lake kwa ajili yetu. Maisha ni safari ya uhusiano na Yesu, kufuatana naye kila hatua. Tunakuwa na maisha yenye furaha na kuzaa matunda katika siku kila mtu anapomfuata. Kujifunza kumfuata Yesu kunahitaji juhudi na mazoezi, kama kujifunza kitu kipya. Kuanza siku kwa sala ya kujisalimisha ni nia nzuri ya kuiweka mioyo yetu kufuata kile Mungu anataka. Ni rahisi kupotea katika safari yetu ya kiroho- kujitenga na mahali tulipo au jinsi upya kurejea kwenye njia sahihi. Tunaweza kupotea au kukwama kwa sababu nyingi, lakini tunahitaji njia rahisi ya kurejea kwenye safari. Watu wengine wanasubiri kufanya hivyo katika ibada inayofuata au kwenye masomo ya Biblia. Wakati mwingine lazima kuwe na tukio baya. Lakini hatuhitaji kusubiri kufanywa upya katika safari yetu. Hapa kuna niia nyepesi ya kuiweka mioyo yetu sawa. Kama uliwahi kucheza mchezo wowote, unajua kwamba kila mtu ana nafasi ya kuwa tayari ama kuanza. Ni nafasi nzuri ya kuanza kufanya kila kinachokuja mwanzo. Ni nafasi ya kiroho kuachilia kitendo chochote- nenda, fanya, sema, au toa- kile ambacho Yesu anakutaka siku hiyo, kulingana na nguvu ya Roho Mtakatifu ikaayo ndani yako kuliko kujitahidi kwa nguvu zako mwenyewe. Maombi ni njia rahisi ya kulinganisha moyo wako na wake, macho yako yakimuangalia yeye, miguu yako ikiwa tayari kumfuata na mikono yako ikiwa tayari kumtumikia kwa njia yoyote atakayokuongoza leo. Kama hujafanya hivyo, unaweza kuinama mbele ya Yesu na kwa nguvu za Roho Mtakatifu utakwenda, utafanya, utasema na kutoa kwa ajili ya heshima na utukufu wake? Sasa, lifanye hili kuwa ni zoezi la kila siku kujisalimisha kwake. Na kwa nini usimwambie rafiki yako uamuzi wako na kuwatia moyo kufanya kama ulivyofanya. Hongera kwa kumaliza safari hii ya siku 7 ya kuingia ndani zaidi katika kujisalimisha kwaYesu! Ukitaka kujifunza zaidi kuhusu maombi haya na jinsi ya kutembea katika kujisalimisha kwa Yesu
siku 6

Kuhusu Mpango huu

Go Do Say Give: The Freedom Of Surrender To Jesus

Kujisalimisha kwa Yesu ni tukio kubwa maishani. Lakini uamuzi huu unamaanisha nini na tutauishi vipi kila siku? Uamuzi ni wa mambo makubwa ya maisha pekee, ama wacha Mungu kupita kiasi? Woga, makosa yaliyopita, na kutoelewa vinaweza kutuzuia.  "Nenda Tenda Sema Toa" ni ahadi/sala ambayo inafunua jinsi utakavyochukua hatua zinazofuata katika safari yako ya kiroho. Pata uhuru unaotokana na kumfuata Yesu. 

More

Tungependa kushukuru Cru kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.cru.org/us/en/pledge.html