Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Nenda Tenda Sema Toa: Uhuru wa Kujisalimisha kwa YesuMfano

Go Do Say Give: The Freedom Of Surrender To Jesus

SIKU 4 YA 7

Nitafanya Unachotaka Nifanye

Kufanya Mungu anachohitaji tufanye inaweza kuogopesha, kama vile tunamualika Mungu kutupa kitu kikubwa cha kufanya ambacho hatuwezi kumaliza. Kuna vitu vingapi vya sisi kufanya? Tunaanzia wapi kutii amri za Yesu?

Kitu kimoja kipo wazi kutoka kwenye injili ni kwamba watu hawahisi sawa kuhusu Yesu kama Mafarisayo. Mafarisayo walifanya haki kuwa ngumu na isiyopatikana na labda isiyotakiwa. Kwenye mahubiri yake mlimani, Yesu alirahisisha yote, kuweka katika sentensi moja juu ya tunacho takiwa kufanya: "Kwa hiyo cho chote ambacho ungependa watu wakutendee, na wewe watendee vivyo hivyo, hii ndio sheria na manabii" (Matayo 7:12).

Hii inaweza kuogopesha, lakini fikiria siku yako leo: unaweza kukutana na watu wa aina zote unapofanya kazi, au kwenda darasani, au kuhudumia familia yako, au kushughulika na maisha ya kawaida kiujmla. Unaweza kuungana na watu kwenye mtandao. Ndipo kuna mwingiliano wa kawaida unavyo endelea na shughuli za kila siku?

Kwenye kila mwingiliano, unapenda kutendewaje?  Kufanya Yesu anachotaka tufanye ina maanisha hivyo ndo jinsi ya kuwatendea. Mika 6:8b inatupa aina tatu ambayo inatusaidia kufikiria kwa vitendo cha kufanya: kutenda kwa wengine sawa na bila upendeleo, kuonesha rehema kwa wanaohitaji, na kuishi kwa unyenyekevu kwa Mungu kwa kuto kujiweka kama wakubwa au wa muhimu zaidi kuliko wengine.

Ni rahisi kufikiriaMungu anachotaka tufanye zaidi inahusu vitu vya kipekee labda katika wakati wa shida. Lakini zaidi kikawaida, na kinachorukwa, ni kufanya anachotaka katika wakati bila kutambuliwa. Yale matendo madogo madogo, ya kila siku ya kujisalimisha hukomaza imani na bidii yetu, na hutuandaa katika matendo anayopenda tufanye wakati wa mambo yakiwa juu. Inaweza kuwa rahisi kama kufata dhamira, haswa kufanya kitu kinachohusisha sadaka au urahisi binafsi.

<1>Utamuomba Mungu kwa uwezo na busara ya kufanya achotaka ufanye leo? Sali kuhusu kila kitu kwenye ajenda yako ya leo na muombe Mungu akupe uwezo kufanya anachopenda ufanye.

siku 3siku 5

Kuhusu Mpango huu

Go Do Say Give: The Freedom Of Surrender To Jesus

Kujisalimisha kwa Yesu ni tukio kubwa maishani. Lakini uamuzi huu unamaanisha nini na tutauishi vipi kila siku? Uamuzi ni wa mambo makubwa ya maisha pekee, ama wacha Mungu kupita kiasi? Woga, makosa yaliyopita, na kutoelewa vinaweza kutuzuia.  "Nenda Tenda Sema Toa" ni ahadi/sala ambayo inafunua jinsi utakavyochukua hatua zinazofuata katika safari yako ya kiroho. Pata uhuru unaotokana na kumfuata Yesu. 

More

Tungependa kushukuru Cru kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.cru.org/us/en/pledge.html