Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Nenda Tenda Sema Toa: Uhuru wa Kujisalimisha kwa YesuMfano

Go Do Say Give: The Freedom Of Surrender To Jesus

SIKU 2 YA 7

Kwa nguvu ya Roho Mtakatifu

Fikiria uko kwenye safari ndefu ya maisha yako, lakini uko peke yako. Hakuna wa kusema naye, hakuna wa kukusaidia, na hakuna wa kufurahia naye. Hii itakuwa safari ngumu na ya kuhuzunisha. Bahati mbaya, wakristo wengi wanaishi maisha haya kwa kutokuona nguvu na faraja ambayo imeahidiwa kupitia Roho Mtakatifu. Kwa namna yoyote, wengi wanasafiri safari zao kana kwamba Yesu hayuko ndani yao.

Matokeo yake, tunasafiri safari zetu kwa juhudi zetu binafsi.Mazingira yetu ya kujitoa na kufanya kazi kwa bidii ili kuwa kama Yesu yanaishia kukatisha tamaa. Maisha ya kujisalimisha kwa Mungu kwa njia hii yataishia kujisikia kama maisha yanayoelekea kwenye kushindwa na kukata tamaa.

Katika Yohana13-17, baada ya miaka mitatu ya kuwa na wanafunzi wake karibu kila siku ya maisha yao, Yesu anawaanda kwa maisha pasipo uwepo wake wa kimwili--ambao ndiyo sisi wafuasi wake tunauona leo. Mara kwa mara alisema nao kuhusu Roho Mtakatifu. Roho atakaa ndani yao na atakuwa nao milele. Anamwita Roho Mtakatifu Roho wa kweli, msaidizi, yeye atakayesema habari za Yesu, yeye atakayewajulisha juu ya dhambi, na atakayewaongoza katika kweli yote.

Katika Yohana 15, Yesu anaelezea hili kwa njia ya mfano wa mzabibu na matawi. Anaita huku kuungana naye kila siku kama "kukaa". Yeye ni mzabibu na sisi ni matawi. Tunatakiwa kukaa, au kufanya makazi yetu ndani yake kwa kuungama dhambi zetu na kuunganishwa naye na maisha yake na nguvu. Hili linawezekana kwa sababu Roho Mtakatifu anakaa ndani yetu. Maisha yake yanatiririka ndani yetu tunapokuwa tumeunganishwa naye, kama vile utomvu ndani ya mzabibu unavyoshuka kweenye matawi. Hatujaachwa wenyewe kwenye safari yetu.

Roho Mtakatifu hufanya kazi kupitia kwetu ili kutubadilisha tabia yetu. Kaama vile matawi, tunapokaa ndani ya Yesu, mzabibu, tutazaa matunda kwa kukaa ndani ya Yesu. Tunasisitiza kukaa, na kuzaa matunda kwa mkristo kunaanza kutokea. Tutachanganyikiwa tunapoangalia katika kujaribu kuzaa matunda, na kusahau kukaa.

Kuzaa matunda mengi, pia kunajulikana kama kukomaa, inachukua muda. Kuwa mvumilivu mwenyewe na wengine katika safari--matunda yatakuja.

Je utadai kwa imani nguvu ya Roho kujaza maisha yako na Yesu leo? 

Chukua muda mchache sasa hivi na utubu dhambi unazozijua; ndipo umwombe Yesu ayajaze maisha yako upya naRoho wake.

siku 1siku 3

Kuhusu Mpango huu

Go Do Say Give: The Freedom Of Surrender To Jesus

Kujisalimisha kwa Yesu ni tukio kubwa maishani. Lakini uamuzi huu unamaanisha nini na tutauishi vipi kila siku? Uamuzi ni wa mambo makubwa ya maisha pekee, ama wacha Mungu kupita kiasi? Woga, makosa yaliyopita, na kutoelewa vinaweza kutuzuia.  "Nenda Tenda Sema Toa" ni ahadi/sala ambayo inafunua jinsi utakavyochukua hatua zinazofuata katika safari yako ya kiroho. Pata uhuru unaotokana na kumfuata Yesu. 

More

Tungependa kushukuru Cru kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.cru.org/us/en/pledge.html