Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Nenda Tenda Sema Toa: Uhuru wa Kujisalimisha kwa YesuMfano

Go Do Say Give: The Freedom Of Surrender To Jesus

SIKU 6 YA 7

Nitatoa kile unachotaka nitoe.
Mungu aliupenda ulimwengu sana hata akamtoa mwane wa pekee kwa ajili ya kutuokoa. Kutoa ni msingi wa moyo wa Mungu kwa ajili ya watu wake. Upendo wa Mungu umefungamana sana na utoaji ndiyo maana haiwezekani kufikiria juu ya upendo bila utoaji. Kumfuata Yesu kutatufikisha maeneo ya utoaji ambayo hatujawahi kuyaona.
Yesu alijua mvuto wa fedha ndiyo maana alikuwa na ujumbe mzito kwa ajili yetu:" Hakuna mtu awezaye kutumikia mabwana wawili, kwa maana atamchukia huyu na kumpenda huyu, au atajitoa sana kwa huyu na kumdharau huyu. Hamwezi kumtumikia Mungu na mali" (Mathayo6: 24). Tamaa ya fedha ina nguvu sana ndani yetu na inaweza kutuzuia kumfuata Mungu kikamilifu.
Tunawezaje kushinda hiyo nguvu? Inakuja kwa njia ya kuiacha, na kama masuala mengine ya maombi haya, ni suala ya moyo. Hatujaambiwa kwamba kuwa na fedha ni vibaya au dhambi. Kupenda fedha ndiyo tatizo. Na kila tulichonacho ni mali yake. Tumepewa kutunza kwa muda tuu mali za ufalme wake, na kuwekeza mali hizo zinapoliheshimu jina lake. Kwa hiyo hakuna chochote nilichonacho kilichochangu na kufanya ninavyotaka.
Moja ya somo kwa wana wa Israeli walipokuwa wanazunguka jangwani kwa miaka arobaini ilikuwa ni kwamba Mungu alikuwa mkweli kwa ahadi yake ya kuwapa mkate wa kila siku kutoka mbinguni. Yesu alituagiza tuombe mkate wa kila siku. Mungu anawaangalia watu wake kila siku. Anataka tuone utoaji wa mahitaji yetu ya kila siku ya maisha yetu. Hilo litatusaidia kumpa kwa moyo mkunjufu na kuwapa wengine anachotaka tutoe- si fedha pekee, bali hata maisha yetu.
Warumi 12:1 inasema kwamba " yatupasa kuitoa MIILI yetu kama dhabihu iliyo hai, takatifu, ya kumpendeza Mungu, ndiyo ibada YETU yenye maana. Mfano ni mfumo wa ibada za kujitoa katika Agano la Kale. Yatupasa kutoa maisha yetu yote madhabahuni mbele za Mungu, ikiwa ni pamoja na fedha tunazopata.
Kutoa kwa ukarimu kunatoka kwenye moyo wa ukarimu wenye shukrani kwa Mungu. Hebu tafakari kwa muda juu ya jambo au mtu ambaye Mungu amemuweka moyoni mwako umsaidie kifedha au kwa muda wako.
Je, utatoa kile Mungu anakutaka utoe leo
siku 5siku 7

Kuhusu Mpango huu

Go Do Say Give: The Freedom Of Surrender To Jesus

Kujisalimisha kwa Yesu ni tukio kubwa maishani. Lakini uamuzi huu unamaanisha nini na tutauishi vipi kila siku? Uamuzi ni wa mambo makubwa ya maisha pekee, ama wacha Mungu kupita kiasi? Woga, makosa yaliyopita, na kutoelewa vinaweza kutuzuia.  "Nenda Tenda Sema Toa" ni ahadi/sala ambayo inafunua jinsi utakavyochukua hatua zinazofuata katika safari yako ya kiroho. Pata uhuru unaotokana na kumfuata Yesu. 

More

Tungependa kushukuru Cru kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.cru.org/us/en/pledge.html