Ninakungoja Hapa, Njia ya Majirio ya TumainiMfano
UNYENYEKEVU UNAONEKANA MZURI KWA KILA MTU
TAFAKARI
Yesu ni Mfalme wa Wafalme, lakini alikuja kama mtumishi mnyenyekevu. Unyenyekevu si kujizania mnyonge, pasipo kusahau ukweli kwamba ni Yesu aliyekufanya uwe juu. Sasa unafananaje na Yesu? Unajengaje roho ya unyenyekevu?
Unyenyekevu ni matunda ya kuwa na Yesu. Yeyote anayetembea kwa karibu na Yeye hawezi kujifikiria kuwa juu zaidi ya anavyotakiwa. Kupendwa na Yesu na kualikwa katika uhusiano naye, ndicho tunachotaka na kupata upole na neema yake.
Kuwa mnyenyekevu haimaanishi wewe ni dhaifu. Mungu amekupa yote unayoyahitaji kuishi vizuri kama mwana wake. Wenye kiburi kamwe hawawezi kuliinua jina la Mungu katika sifa. Lakini bado huwainua wanyenyekevu kwenye viwango vipya.
TAFAKARI NA OMBI
Liturgia Binafsi ya Unyenyekevu
Yesu, niokoe na shauku ya kusifiwa.
Yesu, niokoe na shauku ya kuheshimiwa.
Yesu, niokoe na shauku ya kuchaguliwa.
Yesu, niokoe na shauku ya kuulizwa ushauri.
Yesu, niokoe na shauku ya kukubalika.
Yesu, niokoe na shauku ya faraja na utulivu
Yesu, niokoe na hofu ya kudhalilishwa.
Yesu, niokoe na hofu ya kushutumiwa.
Yesu, niokoe na hofu ya kupitwa.
Yesu, niokoe na hofu ya kusahaulika.
Yesu, niokoe na hofu ya kuwa mpweke.
Yesu, niokoe na hofu ya kuumizwa.
Yesu, niokoe na hofu ya mateso.
Kwamba wengine wapendwe zaidi yangu,
Yesu, nipe neema ya kutamani hivyo.
Kwamba wengine wachaguliwe na mimi niachwe,
Yesu, nipe neema ya kupenda hivyo.
Kwamba wengine wasifiwe na mimi nisionekane,
Yesu, nipe shauku ya kutamani hivyo.
O Yesu, mpole na mnyeyekevu wa moyo, ufanye moyo wangu kama wako,
O Yesu, mpole na mnyenyekevu, nitie nguvu kwa Roho wako.
O Yesu, mpole na mnyenyekevu wa moyo, nifundishe njia zako.
nisaidie kuweka umuhimu wangu pembeni
kujifunza aina ya ushirikiano na wengine
ambao wanafanya uwepo wako uwezekane katika nyumba Abba. Amen.
Yesu
Imechukuliwa kwenye ombi la Rafael,
Cardinal Merry Del Val, 1865–1930
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Majirio ni majira ya matarajio na maandalizi. Ungana na mchungaji na mwandishi Louie Giglo katika safari ya majirio kupata ufahamu ya kuwa kungojea siyo kuharibu hasa unapomngojea Bwana. Shikilia nafasi ya kupata ufunuo na tumaini katika safari hii ya majirio. Katika siku saba zijazo utapata amani na himizo kwa nafsi yako kama vile matarajio kuelekea sherehe!
More