Ninakungoja Hapa, Njia ya Majirio ya TumainiMfano
YESU NI KARAMU YETU
TAFAKARI
Yesu hakupi tuu unachohitaji; Yesu ndicho unachohitaji. Moyo wako uliumbwa na Yeye, kwa ajili yake. Unaweza kupigana na kujitahidi kuupata ulimwengu, lakini bila Yesu, huwezi kutosheka kikamilifu.
Kama kuna kutotosheka kunakoongezeka ndani ya moyo wako--njaa ambayo haijatoshelezwa na watu, anasa, sherehe, mali, au mafanikio--leo ndiyo leo kufungua moyo wako kwa wazo la kwamba uliumbwa kwa ajili ya Yesu. Lakini yakupasa kuondoka kwenye "upungufu" na kumwomba Yeye kufanyika "vyote" kwako. Yesu anatosha kwako, na yuko hapa.
TAFAKARI
Njoo, Njoo, Emmanueli
Njoo, Njoo, Emmanueli,
Fidia kwa Israeli mateka
Inayoomboleza katika upweke uhamishoni hapa
Mpaka mwana wa Mungu atokee.
Furahi, Furahi!
Emmanueli atakuja kwako, O Israeli.
Njoo, Ee Tawi la shina la Yese
Kwa walio wako na uwaokoe!
Kutoka vilindi vya kuzimu uwaokoe watu wako,
Na uwape ushindi dhidi ya kaburi.
Furahi! Furahi!
Emmanueli atakuja kwako, O Israeli.
Kiyunani, c. Karne ya 12
Psalteriolum Cantionum Catholicarum, Köln, 1710
Imetafsiriwa na John Mason Neale, 1818–1866, alt.
Fungu la 1 & 4
OMBI
Baba, wewe pekee unajua ni kiasi gani nimetafuta utoshelevu kwa watu na vitu vya dunia hii. Vyote vimevunjika na mimi vilevile. Wewe pekee unaweza kuushibisha moyo wangu wenye njaa. Wewe pekee una upendo usiolinganishwa. Hubadiriki. Fungua macho yangu leo. Nionyeshe utajiri wako na utukufu wako. Nisaidie kukujua zaidi. Hebu nione karamu yako iliyoandaliwa mbele yangu, ili nijifurahishe katika wewe. Amen.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Majirio ni majira ya matarajio na maandalizi. Ungana na mchungaji na mwandishi Louie Giglo katika safari ya majirio kupata ufahamu ya kuwa kungojea siyo kuharibu hasa unapomngojea Bwana. Shikilia nafasi ya kupata ufunuo na tumaini katika safari hii ya majirio. Katika siku saba zijazo utapata amani na himizo kwa nafsi yako kama vile matarajio kuelekea sherehe!
More