Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Ninakungoja Hapa, Njia ya Majirio ya TumainiMfano

Waiting Here for You, An Advent Journey of Hope

SIKU 3 YA 7

NIMUOGOPE NANI?

TAFAKARI

Katikati ya chuki na ghadhabu, wewe mwangalie Yesu. Anakupigania. Emmanueli yuko karibu. Ijapokuwa mashitaka yanakuja na adui anashambulia mawazo yako, ijapokuwa watu wanajaribu kukuangusha na kuchafua jina lako, ijapokuwa mipango inafanyika na majaribu yanakuja, ijapokua mwili unataka kulipiza kisasi --tumaini lako liko kwake yeye anayekupigania. Uko salama katika upendo wa Mungu na katika nguvu ya jina lake lenye nguvu.

TAFAKARI

Usiogope Kuniamini Katikati ya Dhoruba

Usiogope kuniamini katikati ya dhoruba,
Siku zote niko karibu sana.
Ninakuja kutuliza hofu yako,
Ndipo, wenye kuchoka, hawaogopi.

Jizuie

Usiogope, niko pamoja nawe,
Usiogope, niko pamoja na wewe,
Usiogope, niko pamoja na wewe,
Niko pamoja na wewe siku zote.

Siku zote naweza nisionekane kama niko karibu
Kama ambavyo natakiwa kuwa;
Lakini katikati ya dhoruba na utulivu,
Ninaona hatari zako zote.

Jizuie

Usiogope kuutumaini mkono wangu wenye nguvu;
Ulileta wokovu duniani.
Niliteseka sana kukupa uzima,
Kukupa taji.

Jizuie

J.W. Howe, Beti la 1–3

OMBI

Baba, katika ya dhoruba ninaweka tumaini langu kwako. Unanipigania na wewe ni mkubwa kuliko maadui zangu. Hakuna nachokutana nacho leo kina nguvu zaidi yako. Wewe ni mwamba imara chini ya miguu yangu. Asante kwa kuwazunguka wale wanaonizunguka. Nipe amani mbele ya adui zangu, nikijua unanitazama na unanilinda katika upendo wako. Amen.

siku 2siku 4

Kuhusu Mpango huu

Waiting Here for You, An Advent Journey of Hope

Majirio ni majira ya matarajio na maandalizi. Ungana na mchungaji na mwandishi Louie Giglo katika safari ya majirio kupata ufahamu ya kuwa kungojea siyo kuharibu hasa unapomngojea Bwana. Shikilia nafasi ya kupata ufunuo na tumaini katika safari hii ya majirio. Katika siku saba zijazo utapata amani na himizo kwa nafsi yako kama vile matarajio kuelekea sherehe!

More

Tunapenda kumshukuru Louie Giglio, mwandishi wa Waiting Here for You (Passion Publishing), kwa kutoa mpango huu. Kwa taarifa zaidi, tafadhali tembelea: www.passionresources.com