Ninakungoja Hapa, Njia ya Majirio ya TumainiMfano
NI WAKATI SAHIHI
TAFAKARI
Mwokozi aliahidiwa kwa watu wa Mungu kwa karne nyingi. Walitamani na kuomba kwa ajili ya ukombozi. Ndipo kwa siku sahihi, mahali sahihi, wakati sahihi, Yesu alizaliwa. Ni mara chache Mungu huja wakati tunapomhitaji, siku zote huja wakati sahihi.
Sisi wote tunasubiri jambo, mara nyingi tukijiuliza kama Mungu ametusahau. Katika kungoja kwako, hebu kuzaliwa kwa Yesu kukutie moyo. Kwa sababu tu Mungu hajaja ( kama unavyoweza kuona), haimaanishi amekuacha. Kwake siku moja ni kama miaka elfu na miaka elfu ni kama siku moja. Hata dakika hii anafanya kwa utukufu wake na kwa ajili yako. Japo mazingira yanasema tofauti, Mungu ataonekana, kwa ratiba yake, akitimiza mipango yake ya muda mrefu kwa ajili yako. Usikate tamaa wakati ni sasa.
Tumaini katika hori la kulia ng'ombe na ujue unapendwa na kuthaminiwa na Mungu aliyeshuka kutoka mbinguni na alifika kwa wakati sahihi kwa ajili yako.
TAFAKARI
Sikiliza Sauti ya Furaha
Sikiliza sauti ya furaha! Mwokozi anakuja,
Mwokozi aliyeahidiwa zamani;
Kila moyo uandae enzi,
Na kila sauti wimbo.
Anakuja na kufungulia wafungwa,
Waliofungwa na shetani.
Milango ya chuma ikivunjika mbele yake,
Makomeo yote yakiyeyuka.
Anakuja kufunga mioyo iliyovunjika,
Kuponya nafsi zinazotoka damu,
Na hazina ya neema yake
Kuwatajirisha masikini wanyenyekevu.
Hosanna wetu wa furaha, Mfalme wa Amani,
Tutatangaza ujio wako,
Na utajiri wako wa milele mbinguni hushangilia
kwa jina lako pendwa.
Philip Doddridge, 1702–1751
OMBI
Baba, kutana nami ninapokungoja, mahali napotamani kitu ambacho hakionekani waziwazi. Tuliza moyo wangu na unipe uwezo wa kujua kwamba uko karibu. Naamini mipango yako ni mizuri. Ninaiona katika kuzaliwa kwa mwana wako.
Lakini wakati mwingine nahangaika kuangalia zaidi ya ukungu unaonizunguka. Zidisha ujasiri wangu ninapoinua macho yangu kwako. Utukuzwe katika maisha yangu wakati huu wa majira ya matarajio. Amen.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Majirio ni majira ya matarajio na maandalizi. Ungana na mchungaji na mwandishi Louie Giglo katika safari ya majirio kupata ufahamu ya kuwa kungojea siyo kuharibu hasa unapomngojea Bwana. Shikilia nafasi ya kupata ufunuo na tumaini katika safari hii ya majirio. Katika siku saba zijazo utapata amani na himizo kwa nafsi yako kama vile matarajio kuelekea sherehe!
More