Ninakungoja Hapa, Njia ya Majirio ya TumainiMfano
UTUKUFU JUU MBINGUNI
TAFAKARI
Mungu hana wa kulingana naye. Hakuna kupungukiwa. Hakuna mahitaji. Yuko mbele ya kila kitu na mwisho wa siku atakuwa wa mwisho amesimama. Ulimwengu umejaa "m ndogo" miungu, lakini Mungu wetu alifanya mbingu na nchi. Hakuna wa kulinganisha na Yeye. Wala hakuna wa kumkaribia.
Kwa hiyo unapomngoja leo, mpe sifa. Yawezekana mazingira yako yanaonekana kuwa juu chini, lakini kiti chake cha enzi kipo juu! Msifu ukiwa katika kusubiri. Muinue katika kutangatanga kwako. Kwa hiyo usiombe mambo mengi leo, endelea kuliinua jina lake juu ya majina yote. Acha jina hilo lisimike moyo wako na kutuliza nafsi yako. Acha sifa zako ziwafunike wengine wote wanaoshindana kwa ajili ya utii na upendo wako. Utakapofanya hivyo, wimbo wako utainua mawazo yako hata mahali pa juu.
TAFAKARI
Utukufu juu mbinguni
Wewe ni wa kwanza
Unatangulia
Wewe ni wa mwisho
Bwana, wewe ni wa kudumu
Jina lako liko kwenye nuru ili kuliona
Nyota mbinguni zinatangaza utukufu wako
Utukufu juu mbinguni
Utukufu juu mbinguni
Utukufu juu mbinguni
Mbali na wewe hakuna mungu
Nuru ya ulimwengu
Nyota ya asubuhi ing'aayo
Jina lako litang'aa wote walione
Ni wewe
Wewe ni utukufu wangu
Na hakuna yeyote unayeweza kulinganisha
Kwako, Bwana
Dunia nzima kwa pamoja inatangaza....
Utukufu mbinguni . . . kwako, Bwana
Dunia yote itaimba sifa zako
Mwezi na nyota, jua na mvua
Kila taifa litatangaza
Kwamba wewe ni Mungu na utatawala
Utukufu, utukufu halleluya
Utukufu, utukufu kwako, Bwana
Halleluya
Chris Tomlin, Matt Redman, Jesse Reeves, Daniel Carson, Ed Cash
OMBI
Baba, niseme nini kwako? Huna wa kufanana nawe au mshindani. Maneno yangu na mawazo yangu ni madogo sana ukilinganisha na wewe. Nimeona nyota za usiku na haziwezi kushika mshumaa kwa utukufu wako. Ongeza imani yangu na unipe maneno napotaka kuungana katika wimbo wa sifa zako.
Sifa zote ni zako, sasa na hata milele. Nitatembea katika kweli hiyo leo. Nitaiamini. Na kuitendea kazi. Na kuomba kama ilivyo. Na kutoa kama ilivyo. Na kusifu kama hakuna kama wewe. Amen!
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Majirio ni majira ya matarajio na maandalizi. Ungana na mchungaji na mwandishi Louie Giglo katika safari ya majirio kupata ufahamu ya kuwa kungojea siyo kuharibu hasa unapomngojea Bwana. Shikilia nafasi ya kupata ufunuo na tumaini katika safari hii ya majirio. Katika siku saba zijazo utapata amani na himizo kwa nafsi yako kama vile matarajio kuelekea sherehe!
More