Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Ninakungoja Hapa, Njia ya Majirio ya TumainiMfano

Waiting Here for You, An Advent Journey of Hope

SIKU 5 YA 7

TULIA

Nyakati za kutulia wakati tukisubiri kwa tumaini katika Bwana.

TAFAKARI

Nyakati za ukimya ni chache na inaweza kuwa vigumu kupata utulivu, lakini chukua dakika chache leo kimyakimya na umtafakari Bwana. Usijaribu kusoma au kujifunza au kuvurugwa--wewe tulia na utafakari juu ya utu wa Yesu na yote aliyofanya kwa ajili yako. Fikiria juu ya kuzaliwa kwake, utoto wake, na mwanga ukitokeza katika ulimwengu wenye giza na uliochoka. Fikiria juu ya mauti yake na sadaka, na zawadi ya uzima wake anayokupa. Tafakari juu ya kufufuka kwake, nguvu yake dhidi ya giza na kaburi. Kunywa uweponi kwake na katika utulivu utafute uso wake. Na fikiria juu ya kuja kwake, siku utakapomuona uso kwa uso.

TAFAKARI

Hebu chukua muda na utulie mbele zake. Fikiria juu ya Yesu na jivike ujasiri katika Yeye.

OMBI

Baba, ninakungoja hapa. Kutana nami katika ukimya. Kutana nami wakati huu. Kutana nami ndani na kupitia kwa mwana wako Yesu na kwa Roho Mtakatifu. Amen.

siku 4siku 6

Kuhusu Mpango huu

Waiting Here for You, An Advent Journey of Hope

Majirio ni majira ya matarajio na maandalizi. Ungana na mchungaji na mwandishi Louie Giglo katika safari ya majirio kupata ufahamu ya kuwa kungojea siyo kuharibu hasa unapomngojea Bwana. Shikilia nafasi ya kupata ufunuo na tumaini katika safari hii ya majirio. Katika siku saba zijazo utapata amani na himizo kwa nafsi yako kama vile matarajio kuelekea sherehe!

More

Tunapenda kumshukuru Louie Giglio, mwandishi wa Waiting Here for You (Passion Publishing), kwa kutoa mpango huu. Kwa taarifa zaidi, tafadhali tembelea: www.passionresources.com