Ninakungoja Hapa, Njia ya Majirio ya TumainiMfano
MUNGU HUFANYA KAZI TUKIWA TUNASUBIRI
TAFAKARI
Kama ni wa kweli, wote tunachukia kusubiri. Kusema ukweli, mara nyingi tunasema kitu kama, " Siwezi kuamini inachukua muda kiasi hiki; inanigharimu muda ambao sina!" Ni kwa sababu wengi wetu tunahesabu kusubiri kama kupoteza muda. Lakini siyo hivyo kwa Mungu wetu.
Mungu hufanya kazi tukiwa tunasubiri. Hata kama huwezi kuona anachokifanya, Mungu siku zote anaamrisha matukio ya mbinguni na duniani kutimiza kusudi lake kwa maisha yako. Amini katika upendo wake usioshindwa-- upendo uliomfanya amtoe Mwokozi kutoka mbinguni kukurejesha na kukuokoa. Mipango ya Mungu kwa maisha yako haiwezi kuzuiliwa. Subiri kwa saburi, ukijua kwamba kusubiri si kupoteza muda ukiwa unamsubiri Mungu.
TAFAKARI
Karibu Yesu Wewe Uliyesubiriwa Muda Mrefu
Karibu, Yesu uliyesubiriwa Muda mrefu
Umezaliwa kuwaweka watu wako huru;
Tufungue kutoka katika hofu na dhambi zetu,
Hebu tupate pumziko katika Wewe
Nguvu na faraja ya Israeli,
Wewe ni tumaini la ulimwengu wote;
Mpenzi Shauku ya kila taifa,
Furaha ya kila moyo wenye shauku.
Ulizaliwa kuwaokoa watu wako,
Ulizaliwa kama mtoto lakini Mfalme,
Ulizaliwa kutawala ndani yetu milele,
Sasa ufalme wako wa neema umetuletea.
Kwa Roho wako wa milele
Tawala katika mioyo yetu wote peke yako;
Kwa sifa zako kamilifu,
Tuinue kwenye kiti chako cha utukufu.
Charles Wesley, 1707–1788
OMBI
Baba, niko hapa nakusubiri. Moyo wangu na mikono yangu iko wazi kwa kusudi lako na mipango ya maisha yangu. Nipe uvumilivu nao uhitaji sana na uniongoze katika kusubiri kwangu. Japo hisia zangu zinaweza kuwa hazipo hapo bado, naamini unafanya kazi kwa niaba yangu hata dakika hii, ukinilinda, ukinihifadhi, ukiniandaa na kunipa mahitaji. Nipe neema ya kuendelea kukuamini katikati ya mawimbi ya mashaka yanayovuma kunizunguka. Tia nanga moyo wangu katika Wewe. Amen.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Majirio ni majira ya matarajio na maandalizi. Ungana na mchungaji na mwandishi Louie Giglo katika safari ya majirio kupata ufahamu ya kuwa kungojea siyo kuharibu hasa unapomngojea Bwana. Shikilia nafasi ya kupata ufunuo na tumaini katika safari hii ya majirio. Katika siku saba zijazo utapata amani na himizo kwa nafsi yako kama vile matarajio kuelekea sherehe!
More