YouVersion Logo
Search Icon

Soma Biblia Kila Siku/AGOSTI 2023Sample

Soma Biblia Kila Siku/AGOSTI 2023

DAY 10 OF 31

Bwana Yesu alisema na kutenda yale yanayoleta sifa na utukufu kwa Mungu, wala ndani yake hakuwa na udhalimu. Alisema, Mafunzo yangu si yangu mimi, ila ni yake yeye aliyenipeleka. Mtu akipenda kuyatenda mapenzi yake, atajua habari ya yale mafunzo, kwamba yatoka kwa Mungu, au kwamba mimi nanena kwa nafsi yangu tu. Yeye anenaye kwa nafsi yake tu hutafuta utukufu wake mwenyewe; bali yeye anayetafuta utukufu wake aliyempeleka, huyo ni wa kweli, wala ndani yake hamna udhalimu(m.16-18). Hakutafuta sifa na utukufu wake binafsi. Aliposifiwa na Wayahudi kwa mafundisho mazuri, hakuvimba kichwa kwa sifa hizo bali aliwaelekeza waliomsifu kwa Mungu na kufichua uovu wao wa kutaka kumwua kwa sababu ya kumponya mtu siku ya sabato. Katika Flp 2:5-7 twasoma:Iweni na nia iyo hiyo ndani yenu ambayo ilikuwamo pia ndani ya Kristo Yesu; ambaye yeye mwanzo alikuwa yuna namna ya Mungu, naye hakuona kule kuwa sawa na Mungu kuwa ni kitu cha kushikamana nacho; bali alijifanya kuwa hana utukufu, akatwaa namna ya mtumwa, akawa ana mfano wa wanadamu. Hakika, nia hii ya Kristo iwemo ndani yetu. Maneno na matendo yetu yajae kumtukuza Mungu.

Scripture

Day 9Day 11

About this Plan

Soma Biblia Kila Siku/AGOSTI 2023

Soma Biblia Kila Siku Agosti 2023 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kuelewa somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu Yohana na Mithali. Karibu kujiunga na mpango huu.

More