YouVersion Logo
Search Icon

Soma Biblia Kila Siku/AGOSTI 2023Sample

Soma Biblia Kila Siku/AGOSTI 2023

DAY 13 OF 31

Yesu ni Mwokozi wa ulimwengu na ni mwalimu bora sana. Hapa ameketi akitoa mafundisho yanayopenya rohoni. Linganisha na ilivyoandikwa kuwaalipokuwa ameketi nao chakulani, alitwaa mkate, akaubariki, akaumega, akawapa. Yakafumbuliwa macho yao, wakamtambua; kisha akatoweka mbele yao. Wakaambiana, Je! Mioyo yetu haikuwaka ndani yetu hapo alipokuwa akisema nasi njiani, na kutufunulia maandiko?(Lk 24:30-32). Ghafla wajaribu wanaingilia kati! Lakini kwa neno moja anawafunulia unafiki na ujinga wao wa kutojua neno la Mungu. Pia anamwokoa yule mwanamke aliyesemwa kufumaniwa na washitaki wake. Kwa kumwonya yule mwanamke kutotenda dhambi tena na kuwanyamazisha washtaki wakatili, Yesu anajidhihirisha kuwa Bwana na Mtawala wa Haki. Tulia na kumsikiliza Bwana Yesu kila siku.

Scripture

Day 12Day 14

About this Plan

Soma Biblia Kila Siku/AGOSTI 2023

Soma Biblia Kila Siku Agosti 2023 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kuelewa somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu Yohana na Mithali. Karibu kujiunga na mpango huu.

More