YouVersion Logo
Search Icon

Soma Biblia Kila Siku/AGOSTI 2023Sample

Soma Biblia Kila Siku/AGOSTI 2023

DAY 12 OF 31

Siku kubwa ya Sikukuu ya Vibanda maandamano yalifanyika Yerusalemu, maji yakiletwa kutoka chemchemi fulani mpaka hekaluni. Hapohapo Yesu anatangaza habari ya maji yaliyo hai ambayo ni mfano wa Roho Mtakatifu. Bila Roho huyo tu vipofu na viziwi kama Mafarisayo. Anapatikana wapi? Kwa Yesu! Alipotukuzwa, kwanza msalabani, halafu mbinguni alipopaa, Yesu alitufungulia kupewa Roho Mtakatifu. Tu heri tukiisikia sauti yake asemapo: “Mtu akiona kiu, na aje kwangu anywe.” Twende kwa Yesu!

Scripture

Day 11Day 13

About this Plan

Soma Biblia Kila Siku/AGOSTI 2023

Soma Biblia Kila Siku Agosti 2023 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kuelewa somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu Yohana na Mithali. Karibu kujiunga na mpango huu.

More