YouVersion Logo
Search Icon

Soma Biblia Kila Siku/ Aprili 2023Sample

Soma Biblia Kila Siku/ Aprili 2023

DAY 19 OF 30

Musa alipofikia umri wa miaka 40, alipata wazo kwamba Mungu amemchagua ili awaokoe Waisraeli katika utumwa wa Misri; lakini tendo lake la haraka la kumwua Mmisri aliyempiga Mwebrania lilionesha kwamba bado hajawa tayari kwa kazi aliyokusudiwa na Mungu. Wala watu wake hawakuwa tayari kumtambua yeye kuwa mwokozi wao kwa wakati huo. Ili kuokoa maisha yake, Musa alitoroka Misri na kukimbilia Midiani. Kwa kufanya hivyo alikataa kwa makusudi hali yake na cheo chake huko Misri. Kwa imani Musa alipokuwa mtu mzima, akakataa kuitwa mwana wa binti Farao;akaona ni afadhali kupata mateso pamoja na watu wa Mungu kuliko kujifurahisha katika dhambi kwa kitambo (Ebr 11:24-25).

Day 18Day 20

About this Plan

Soma Biblia Kila Siku/ Aprili 2023

Soma Biblia Kila Siku/Aprili 2023 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Machi pamoja na maelezo machache ya kukusaidia kuelewa zaidi neno ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Yohana, Mithali na Kutoka. Karibu kujiunga na mpango huu bure

More