YouVersion Logo
Search Icon

Soma Biblia Kila Siku/ Aprili 2023Sample

Soma Biblia Kila Siku/ Aprili 2023

DAY 17 OF 30

Farao alijaribu kutawala Waebrania kwa njia ya kuwaua watoto wachanga wa kiume wakati wazaliwapo ili wasiongezeke. Lakini hila zake hazikufanikiwa kwa sababu ya ujasiri wa wakunga waliowasaidia wanawake wa Kiebrania wakati wa kujifungua. Wakunga hao walimcha Mungu; naye Mungu akawabariki wao na familia zao. Pamoja na kushindwa kwa mpango wa kwanza, Farao aliendelea kuagiza watu wake kuwatupa mtoni watoto wa kiume watakaozaliwa. Mpendwa, uwe makini, kwani shetani hachoki kuwasumbua watu wa Mungu.

Day 16Day 18

About this Plan

Soma Biblia Kila Siku/ Aprili 2023

Soma Biblia Kila Siku/Aprili 2023 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Machi pamoja na maelezo machache ya kukusaidia kuelewa zaidi neno ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Yohana, Mithali na Kutoka. Karibu kujiunga na mpango huu bure

More