BibleProject | Ufalme Unaoenda Kinyume na Matarijio / Sehemu ya 2 - Matendo ya MitumePrøve
Njiani kuelekea Roma, mashua iliyokuwa imembeba Paulo inakumbwa na dhoruba kali. Kila mtu aliye humo anahofia maisha yake, isipokuwa Paulo aliye chini ya staha akishiriki chakula kama tu Yesu alivyofanya usiku kabla ya kushtakiwa kwake. Paulo anabariki na kuumega mkate, akiahidi kuwa Mungu yuko nao katika dhoruba. Siku inayofuata, mashua inaharibikia kwenye miamba na kila mtu anasombwa na maji na kupelekwa pwani akiwa salama. Wako salama, lakini Paulo bado amefungwa kwa minyororo. Anapelekwa Rumi na anawekwa chini ya kufungo cha nyumbani. Lakini hali si mbaya sana kwa sababu Paulo anaruhusiwa kukaribisha vikundi vikubwa vya Wayahudi na wasio Wayahudi ili kushiriki nao habari njema kuhusu Yesu, Mfalme aliyefufuka. Cha kushangaza, Ufalme mbadala unaoenda kinyume na matarijio wa Yesu unakua katikati ya kuteseka kwa mfungwa ndani ya Ruma. Katikati ya ufalme mkuu zaidi wa ulimwengu wa wakati huo. Na kwa tofauti hizi kati ya falme, Luka anakamilisha maelezo yake kana kwamba ni sura moja tu katika seimulizi ndefu zaidi. Kwa mbinu hii, Luka anafanikiwa kuwasilisha ujumbe kwa wasomaji kuwa, safari ya kuhubiri habari njema haijaisha. Wote wanaomwamini Yesu wanaweza kushiriki katika Ufalme wake, unaoendelea kuenea hadi leo.
Soma, Tafakari, kisha Ujibu:
• Pitia mstari wa mwisho kabisa wa toleo la pili la Luka (Matendo ya Mitume 28:31). Ni nani angefikiri kuwa gereza la Kirumi lingekuwa jukwaa ambalo kupitia kwake Mungu angeeneza ujumbe wake bila kizuizi? Unahisi kuna vipingamizi vinavyokuzuia kupokea na kushirki na wengine upendo wa Mungu? Labda ni tatizo sugu la afya, uzazi wa mapema, au tatizo la kifedha unalohisi linakusonga. Omba na umwambie Mungu akuonyeshe jinsi anavyotaka ugeuze kizuizi chako juu chini na kukifanya kuwa fursa ya kueneza Ufalme wake. Unapoanza kuona uwezekano, omba ujasiri wa kuutekeleza.
• Unaamini kuwa Yesu ndiye Mfalme mmoja wa kweli na Ufalme wake ni habari njema? Unaweza kushiriki hili na nani? Fikiri kuhusu kualika mtu mmoja au wawili wajiunge nawe kusoma mpango huu. Utaelewa zaidi utakapojifunza kwa mara ya pili na utaweza kushiriki uzoefu wako na marafiki.
Om denne planen
BibleProject ilibuni Ufalme Unaoenda Kinyume na Matarajio Sehemu ya 2 ili kuwatia watu moyo, vikundi vidogo, na familia mbali mbali waweze kusoma Matendo ya Mitume kwa siku 20. Mpango huu unajumuisha video za katuni, mihtasari yenye mawazo yanayojenga, na maswali ya tafakari ili kuwasaidia washiriki kukutana na Yesu na kuzama kwenye ubunifu wa fasihi wa mwandishi na kuelewa na kujifunza kutoka kwenye mtiririko wa mawazo yake.
More