BibleProject | Ufalme Unaoenda Kinyume na Matarijio / Sehemu ya 2 - Matendo ya MitumePrøve

BibleProject | Ufalme Unaoenda  Kinyume na Matarijio  / Sehemu ya 2 - Matendo ya Mitume

Dag 15 av 20

Baada ya vurumai ndani ya Efeso kuisha, Paulo anaondoka na kurejea Yerusalemu kwa wakati kwa ajili ya sikukuu ya Pentekoste ya kila mwaka. Akiwa njiani, anatembelea miji mingi ili kuhubiri habari njema na kuwatia moyo wafuasi wa Yesu. Katika hili, tunaona ulinganifu kati ya Paulo na huduma ya Yesu. Yesu pia alianza safari kwenda Yerusalemu kwa wakati, kwa ajili ya sikukuu ya Wayahudi ya kila mwaka (kwa upande wake, Pasaka) huku akihubiri habari njema ya Ufalme wake njiani. Na kama tu Yesu alivyofahamu kuwa msalaba ulikuwa unamsubiri, Paulo pia anajua kuwa shida na huzuni inamsubiri katika jiji kuu. Kwa hivyo akiwa na maarifa haya, anapanga mkutano wa kuaga. Anawaalika wachungaji kutoka Efeso kukutana naye katika jiji lililo karibu, ambapo anawaonya kuwa mambo yatakuwa magumu zaidi atakapokuwa hayupo. Anawaambia wanafaa kuwa makini ili kuwasadia maskini kwa ukarimu na kulinda na kukuza makanisa yao kwa bidii. Kila mtu anahuzunika kwa kulazimika kumuaga Paulo. Wanalia, wanamkumbatia na kumbusu, na kukataa kuondoka kando yake hadi anapopanda meli yake inayoondoka.

Soma, Tafakari, kisha Ujibu:

• Linganisha maneno ya Paulo katika Matendo ya Mitume 20:23 na maneno ambayo Roho Mtakatifu alimwambia Anania karibu na wakati ambao Paulo alikutana na Yesu aliyefufuka mara ya kwanza (tazama Matendo ya Mitume 9:15-16). Una maswali, maarifa, au mahitimisho yapi unapolinganisha na kutofautisha vifungu hivi viwili?

• Soma maneno ya kuaga ya Paulo (tazama 20:18-35). Unatambua nini? Anawatia moyo, kuwaonya, na kuwaelekeza viongozi wa makanisa ya kwanza kivipi? Unafikiri ni nini kingefanyika ikiwa viongozi wote wangeongoza jinsi Paulo alivyoelekeza? Unawezaje kujibu maelekezo ya Paulo kihalisia leo?

• Yesu alipoanza safari yake kuelekea Yerusalemu, wanafunzi hawakuelewa mateso yaliyokuwa yakimsubiri huko na walijitenga mateso yake yalipojulikana. Lakini Paulo alipoanza safari yake kuelekea jiji kuu, kila mtu alijua kile ambacho kingefanyika na kumuunga mkono kwa moyo mkunjufu. Unafikiri Paulo aliathiriwa vipi na upendo na uungwaji mkono wa wanafunzi? Unaweza kumuunga nani mkono leo?

• Ruhusu kusoma kwako na tafakari ikuchochee kuomba. Dhihirisha shukrani zako kwa Yesu kwa kwenda Yerusalemu na kuteseka kwa ajili yako. Jiombee na uombee viongozi wa kanisa katika jiji lako ili mjiunge na Yesu katika njia zake karimu za kujitolea. Muombe akupatie wazo kuhusu namna unavyoweza kushiriki neema yake na jamii yako wiki hii. Andika mawazo yanayokujia akilini na uyatekeleze.

Dag 14Dag 16

Om denne planen

BibleProject | Ufalme Unaoenda  Kinyume na Matarijio  / Sehemu ya 2 - Matendo ya Mitume

BibleProject ilibuni Ufalme Unaoenda Kinyume na Matarajio Sehemu ya 2 ili kuwatia watu moyo, vikundi vidogo, na familia mbali mbali waweze kusoma Matendo ya Mitume kwa siku 20. Mpango huu unajumuisha video za katuni, mihtasari yenye mawazo yanayojenga, na maswali ya tafakari ili kuwasaidia washiriki kukutana na Yesu na kuzama kwenye ubunifu wa fasihi wa mwandishi na kuelewa na kujifunza kutoka kwenye mtiririko wa mawazo yake.

More