BibleProject | Ufalme Unaoenda Kinyume na Matarijio / Sehemu ya 2 - Matendo ya MitumePrøve

BibleProject | Ufalme Unaoenda  Kinyume na Matarijio  / Sehemu ya 2 - Matendo ya Mitume

Dag 19 av 20

Baada ya Paulo kukata rufaa ili ashtakiwe Rumi, Festo anamweleza Mfalme Agripa yote yaliyofanyika. Hili linamvutia Mfalme na anaamua kuwa anataka kusikia kutoka kwa Paulo yeye mwenyewe. Kwa hivyo siku inayofuata, Luka anatuambia kuwa kila kitu kinapangwa na watawala wengi muhimu wanaandamana na Agripa ili kumsikia Paulo akitoa ushahidi. Kisha Luka anaandika maelezo ya tatu kuhusu simulizi ya Paulo na utetezi wake. Lakini wakati huu, rekodi ya Luka inaonyesha Paulo akishiriki kwa undani zaidi kuhusu kilichofanyika siku aliyokutana na Yesu aliyefufuka. Wakati mwanga unaopofusha ulipong'aa kandokando ya Paulo na akasikia sauti kutoka Mbinguni, ilikuwa ni Yesu akizungumza kwa lahaja ya Kiebrania. Yesu alimuita kuhubiri mabadiliki makuu aliyopitia na Mataifa na Wayahudi, ili wao pia waone mwanga wa msamaha wa Mungu na kutoroka uovu wa Shetani. Paulo alitii amri ya Yesu na kuhubiri ukweli kuhusu mateso na kufufuka kwa Yesu na mtu yeyote atakayesikiliza, akiwaonyesha kutoka kwenye Maandiko ya Kiebrania kuwa Yesu ndiyeMasihi aliyesubiriwa kwa muda mrefu, Mfalme wa Wayahudi. Festo haamini simulizi ya Paulo, na anapiga kelele kuwa Paulo ana kichaa. Lakini Agripa anaona uwiano kwa maneno ya Paulo na anakiri kuwa anakaribia kuwa Mkristo. Japo Festo na Agripa hawakubaliani kuhusu hali ya kiakili ya Paulo, wote wanakubali kuwa Paulo hakufanya chochote kinachostahiki kifo au kufungwa gerezani.

Soma, Tafakari, kisha Ujibu:

• Tafakari kuhusu kinaya chema katika simulizi ya Paulo: kuona kwa kawaida kuliondolewa kwake kwa muda ili aweze kupokea kuona kiroho milele na kushiriki hilo na wengine. Ni maswali, hisia, au mawazo yapi yanakujia akilini unapozingatia hili?

•Pitia kusudi ambalo Yesu alimpatia Paulo kwa makini (tazama Matendo ya Mitume 26:18) na ulinganishe na ombi la Paulo kwa ajili ya kanisa katika Wakolosai 1:9-14. Unatambua nini? Hili linaweza kutuambia nini kuhusu tamanio na kusudi la Yesu kwa wafuasi wake wote?

• Umekaribia kuwa Mkristo? Omba na umwambie Mungu akusaidie kuona ukweli. Muombe akushawishi ujue na upate uzoefu kuhusu Yesu haswa.

•Unamjua mtu yeyote aliyekaribia kuwa Mkristo? Unawezaje kushiriki uzoefu wako kumhusu Yesu naye leo? Chukua muda kumuombea huku ukizingatia maneno ya Paulo katika Matendo ya Mitume 26:29: Mungu naomba ushawishi moyo huu kwa upole ili uone mwanga wa msamaha wako na kupokea tumaini la Ufalme wako.

Dag 18Dag 20

Om denne planen

BibleProject | Ufalme Unaoenda  Kinyume na Matarijio  / Sehemu ya 2 - Matendo ya Mitume

BibleProject ilibuni Ufalme Unaoenda Kinyume na Matarajio Sehemu ya 2 ili kuwatia watu moyo, vikundi vidogo, na familia mbali mbali waweze kusoma Matendo ya Mitume kwa siku 20. Mpango huu unajumuisha video za katuni, mihtasari yenye mawazo yanayojenga, na maswali ya tafakari ili kuwasaidia washiriki kukutana na Yesu na kuzama kwenye ubunifu wa fasihi wa mwandishi na kuelewa na kujifunza kutoka kwenye mtiririko wa mawazo yake.

More