BibleProject | Ufalme Unaoenda Kinyume na Matarijio / Sehemu ya 2 - Matendo ya MitumePrøve

BibleProject | Ufalme Unaoenda  Kinyume na Matarijio  / Sehemu ya 2 - Matendo ya Mitume

Dag 16 av 20

Paulo anavyoendelea kuelekea Yerusalemu, anasimama njiani ili kuitembelea jamii inayokua ya wafuasi wa Yesu. Wote wanajifunza kuhusu nia yake ya kuingia katika jiji kuu na wanaipinga kwa haraka. Wanamuomba asiende, wakiwa na imani kuwa ikiwa ataenda, atafungwa gerezani au kuuawa. Lakini Paulo yuko tayari kufia anachoamini na hivyo anaendelea. Anapofika Yerusalemu, anashiriki katika tamaduni za Kiyahudi ambazo zinawasaidia wengine kuona kuwa hawapingi Wayahudi. Kwa kweli, yeye ni Myahudi mcha Mungu anayempenda Mungu wa baba zake na anaweza kutoa maisha yake kwa ajili ya Myahudi mwenzake. Lakini Wayahudi wanaona Paulo anapochangamana na wasio Wayahudi na wanakasirika. Wanakataa ujumbe wa Paulo, wanamfukuza hekaluni, na kuanza kumpiga hadi kifo.

Warumi wanapokea habari kuwa mambo yanakuwa mabaya Yerusalemu na wanafika kwa muda na kuzuia kipigo cha Paulo kupelekea kifo. Paulo anaondolewa kutoka kwenye umati mkali, na anamshawishi kamanda kumpatia fursa ya kuzungumza na watesaji wake. Akiwa bado amechubuka na kujawa damu kutokana na kipigo, Paulo anaweza kusimama na kuhubiri simulizi yake kwa ujasiri. Anazungumza kwa lahaja ya Kiebrania ili kuwashawishi na kujifananisha na watu wale wale waliokuwa wanataka kumuua. Wanasikiliza kila anachosema hadi anapoanza kuzungumza kuhusu hamu ya Mungu ya kujumuisha Mataifa (wasio Wayahudi) katika mpango wake wa wokovu. Kutokana na hili, umati unaanza kupiga kelele na kutoa matishio ya kifo dhidi ya Paulo. Kuna vurugu, na kamanda wa Kirumi hawezi kuelewa kwanini Wayahudi wanakasirikia Paulo sana kwa kuwaongelea Mataifa. Kwa hivyo kamanda anatambua kuwa lazima kuna mambo fiche yanayochangia hili na kuteswa zaidi kungemfanya ayaseme. Lakini Paulo anazuia kuteswa kwake kukiko kinyume na sheria kwa kufichua kuwa yeye ni raia wa Kirumi. Kamanda anagundua kuwa anaweza kuwa hatarini kwa kumuumiza Mrumi, hivyo Paulo anaachiliwa upesi kutoka rumande na kusindikizwa hadi mahakamani ambapo anaweza kujitetea mbele ya viongozi wa dini waliomshutumu.

Soma, Tafakari, kisha Ujibu:

• Pitia kujitetea kwa Paulo mbele ya umati mkali wa Wayahudi (tazama Matendo ya Mitume 22:1-21). Unatambua nini? Paulo anajifananisha vipi na watesi wake? Unawezaje kujifananisha na maadui zako?

• Paulo alibadilika kutoka kuwatesa watu wanaomfuata Yesu hadi kuwashawishi watu kumfuata Yesu. Umewahi kukutana na mtu aliyebadilika namna hii? Ikiwa ndiyo, unaweza kushiriki simulizi hiyo ya ukombozi na nani leo?

• Badili kusoma kwako na tafakari yako kuwa maombi. Dhihirisha shukrani zako kwa Yesu kwa kujitolea kwake ili kutangaza habari njema kwa watu wote. Jinyenyekeze ili kujifananisha na watu wanaokutendea vibaya, na muombe Mungu aibadilishe mioyo na mawazo ya maadui zako kabisa.

Dag 15Dag 17

Om denne planen

BibleProject | Ufalme Unaoenda  Kinyume na Matarijio  / Sehemu ya 2 - Matendo ya Mitume

BibleProject ilibuni Ufalme Unaoenda Kinyume na Matarajio Sehemu ya 2 ili kuwatia watu moyo, vikundi vidogo, na familia mbali mbali waweze kusoma Matendo ya Mitume kwa siku 20. Mpango huu unajumuisha video za katuni, mihtasari yenye mawazo yanayojenga, na maswali ya tafakari ili kuwasaidia washiriki kukutana na Yesu na kuzama kwenye ubunifu wa fasihi wa mwandishi na kuelewa na kujifunza kutoka kwenye mtiririko wa mawazo yake.

More