BibleProject | Ufalme Unaoenda Kinyume na Matarijio / Sehemu ya 2 - Matendo ya MitumePrøve
Wayahudi wengi walikuwa na matarajio maalumu juu ya Masihi wao. Walifikiri Mfalme wao aliyeahidiwa angechukua kiti cha enzi na kuwaokoa kutoka kwenye ukandamizaji wa Kirumi. Hivyo Yesu alipokuja na kuanza kushirikiana na waliotengwa katika jamii na kutangaza Ufalme wa Mungu kwa unyenyekevu, baadhi hawakumtambua kama Masihi na hata kupinga utawala wake vikali. Kwa kinaya, upinzani wao ulikuwa zana ambayo Mungu alitumia ili kuasisi utawala wa Yesu, na kupitia kusulubishwa, kufufuka, na kupaa mbinguni, Yesu alitawazwa mbinguni kama Mfalme wa Wayahudi na mataifa yote. Katika sehemu inayofuata, Luka anatuambia kile ambacho Paulo alipitia akihubiri ujumbe huu huko Thesalonike, Berea, na Athene.
Akiwa Thesalonike, Paulo alithibitisha kutoka kwenye Maandiko ya Kiebrania kuwa manabii walisema daima kuwa ni lazima Masihi ateseke na afufuke tena ili atawale kama Mfalme. Paulo alionyesha kuwa Yesu alilingana na maelezo hayo ya nabii wa kale, na wengi walishawishika. Jinsi hadhira ya Paulo ilivyokua, baadhi ya Wayahudi wenye wivu waliwachochea washawishi wa jiji wamshutumu Paulo kuwa amebadilisha ulimwengu mzima juu chini na kutangaza Mfalme mpya. Makoloni ya Kirumi hayakutaka kumfadhaisha mfalme, kwa hivyo hii ilikuwa shutuma kali ambayo ingemfanya Paulo auawe. Paulo alitumwa kutoka Thesalonike ili ahubiri habari njema kuhusu Ufalme wa Yesu katika jiji la Berea badala yake. Akiwa huko, Paulo alipata wanaume na wanawake waliokuwa na hamu ya kusikiliza, kusoma, na kuhakikisha kuwa ujumbe wake ulikuwa unalingana na Maandiko ya Kiebrania. Wengi ndani ya Berea walianza kumfuata Yesu, lakini misheni ya Paulo ilifupishwa wakatiWayahudi kutoka Thesalonike walisafiri hadi Berea ili kumfukuza kutoka huko pia. Hili lilimfanya Paulo aende Athene, ambako aliingia katikati ya soko la mawazo ili kueleza utambulisho wa kweli wa “mungu wao asiyejulikana" na maana ya kufufuka kwa Yesu.
Soma, Tafakari, kisha Ujibu:
•Wayahudi walimshutumu Paulo kuwa amegeuza ulimwengu juu chini. Kwa wale wanaopendelea maadili potofu ya falme za ulimwengu, ujumbe wa Ufalme unaoenda kinyume na matarajio unafadhaisha. Lakini njia za Yesu hufadhaisha maadili ya ubinafsi tu ambayo huharibu ulimwengu. Kwa mfano, ni kitu kipi kimoja katika ulimwengu huu kinachohitaji kurekebishwa? Kufuata maadili na mafundisho ya Yesu kutaletaje marekebisho hayo? Ni maadili yapi ya kibinafsi yatahitaji kubadilishwa juu chini ili kuona hilo likifanikishwa?
• Pitia Matendo ya Mitume 17:11-12. Ni mambo yapi mawili mema ambayo Waberea walifanya yaliyowasaidia kufikia uamuzi kuwa kwa kweli Yesu ndiye alikuwa Masiha? Unafikiri ni nini hufanyika ikiwa moja tu kati ya haya mambo mawili hutumika katika mtazamo na matendo ya mtu? Matunda ya ukuaji wako wa kimtazamo na kimatendo katika haya yote yataonekanaje?
• Pitia ujumbe wa Paulo kwa Waathene kwa makini. Anasema nini kuhusu ukaribu wa Mungu na wanadamu na uhusiano wake na ubinadamu? Paulo anasema nini kuhusu utambulisho na kusudi la ubinadamu? Anasema nini kuhusu Yesu? Ujumbe wa Paulo unakuathiri vipi leo?
• Badili fikira zako kuwa ombi. Mshukuru Mungu kwa kukuumba. Mshukuru kwa kujitambulisha na kuwa karibu. Muombe upendo mpya, umakini, na uvumilivu ili uweze kusoma Maandiko na kujifunza habari zake na nguvu ya urejesho ya Ufalme wake.
Skriften
Om denne planen
BibleProject ilibuni Ufalme Unaoenda Kinyume na Matarajio Sehemu ya 2 ili kuwatia watu moyo, vikundi vidogo, na familia mbali mbali waweze kusoma Matendo ya Mitume kwa siku 20. Mpango huu unajumuisha video za katuni, mihtasari yenye mawazo yanayojenga, na maswali ya tafakari ili kuwasaidia washiriki kukutana na Yesu na kuzama kwenye ubunifu wa fasihi wa mwandishi na kuelewa na kujifunza kutoka kwenye mtiririko wa mawazo yake.
More