BibleProject | Ufalme Unaoenda Kinyume na Matarijio / Sehemu ya 2 - Matendo ya MitumePrøve

BibleProject | Ufalme Unaoenda  Kinyume na Matarijio  / Sehemu ya 2 - Matendo ya Mitume

Dag 12 av 20

Luka anaendelea kutuambia kuhusu safari ya misheni ya Paulo kote katika Ufalme wa Rumi. Anavyoendelea kusafiri, anashiriki habari njema kwa ujasiri kuhusu Ufalme wa Yesu na wengi wanasikia ujumbe wa Paulo kama tishio kwa namna yao ya maisha ya Kirumi. Lakini kuna wengine ambao hatimaye wanasikia ujumbe wa Paulo kama habari njema ambazo zinaelekeza kwa namna mpya kabisa ya maisha. Kwa mfano, Luka anatuambia kuhusu mlinzi wa jela kutoka Filipi, tunakutana naye tunapofuatilia simulizi ya kufungwa kimakosa kwa Paulo na Sila.

Baada ya kushutumiwa kusababisha mkanganyiko jiji zima, Paulo na mfanyakazi mwenzake Sila wanapigwa kiuonevu na kufungwa gerezani. Wakiwa macho katika seli yao, huku wamechubuka na kujaa damu, wanaanza kuomba na kumuimbia Mungu. Wafungwa wanasikiliza nyimbo zao za kuabudu wakati tetemeko kubwa la ardhi linakuja na kutetemesha misingi ya gereza hadi minyororo ya wafungwa inavunjika na milango yote ya gereza inafunguka. Mlinzi wa gereza anaona hili na kujua kuwa atauawa kwa kuwaacha wafungwa watoroke, na baada ya kukatia tamaa maisha yake, anachukua upanga wake na kutaka kujiua. Lakini Paulo anamzuia na kuokoa maisha yake. Kutokana na hili, mlinzi huyo mbishi wa gereza anakuwa mtulivu na kuanguka miguuni mwa Paulo na Sila. Anatambua kuwa maisha yake pia yanahitaji kuokolewa milele, na anataka kuijua njia ya wokovu. Paulo na Sila wana hamu kubwa ya kuongea naye, na siku hiyo hiyo mlinzi huyo wa gereza na familia yake yote inaanza kumfuata Yesu.

Soma, Tafakari, kisha Ujibu:

• Milango ya gereza ilifunguliwa. Paulo na Sila wangetoroka na kumwacha mlinzi wa gereza awajibikie matokeo, lakini hawakutoroka. Walisalia katika seli zao gerezani ili kumwokoa mwanaume yule yule aliyewatia humo. Hili linakuambia nini kuhusu tabia yao na nia ya kweli ya misheni yao ya kuhubiri kuhusu Ufalme wa Yesu?

• Tafakari kuhusu namna tulivu Paulo na Sila walimjibu mlinzi huyo wa gereza na jinsi ilivyobadilisha maisha yake (tazama 16:28-34). Ni nani anahitaji jibu lako leo?

•Umekata tamaa katika maisha? Usijiumize; Yesu yuko hapa kwa ajili yako. Anakupenda. Mwamini leo. Mwambie unavyohisi, muombe unachohitaji, na mwalike akuongoze katika njia mpya kabisa ya maisha. Anakusikia.

Dag 11Dag 13

Om denne planen

BibleProject | Ufalme Unaoenda  Kinyume na Matarijio  / Sehemu ya 2 - Matendo ya Mitume

BibleProject ilibuni Ufalme Unaoenda Kinyume na Matarajio Sehemu ya 2 ili kuwatia watu moyo, vikundi vidogo, na familia mbali mbali waweze kusoma Matendo ya Mitume kwa siku 20. Mpango huu unajumuisha video za katuni, mihtasari yenye mawazo yanayojenga, na maswali ya tafakari ili kuwasaidia washiriki kukutana na Yesu na kuzama kwenye ubunifu wa fasihi wa mwandishi na kuelewa na kujifunza kutoka kwenye mtiririko wa mawazo yake.

More