1
Mwanzo 3:6
Biblica® Toleo Wazi Neno: Maandiko Matakatifu 2024
Mwanamke alipotambua kwamba tunda la mti huo lilikuwa zuri kwa chakula na la kupendeza macho, tena linatamanika kwa kujipatia hekima, basi akachuma matunda yake, akala. Pia akampa mumewe, aliyekuwa pamoja naye, akala.
Thelekisa
Phonononga Mwanzo 3:6
2
Mwanzo 3:1
Basi nyoka alikuwa mjanja kuliko wanyama pori wote ambao Bwana Mwenyezi Mungu aliwafanya. Nyoka akamwambia mwanamke, “Ati Mungu alisema, ‘Kamwe msile matunda ya mti wowote wa bustanini’?”
Phonononga Mwanzo 3:1
3
Mwanzo 3:15
Nami nitaweka uadui kati yako na huyu mwanamke, na kati ya uzao wako na wake; yeye atakuponda kichwa, nawe utamuuma kisigino.”
Phonononga Mwanzo 3:15
4
Mwanzo 3:16
Kwa mwanamke akasema, “Nitakuzidishia sana uchungu wakati wa kuzaa kwako; kwa uchungu utazaa watoto. Tamaa yako itakuwa kwa mumeo, naye atakutawala.”
Phonononga Mwanzo 3:16
5
Mwanzo 3:19
Kwa jasho la uso wako utakula chakula chako hadi utakaporudi ardhini, kwa kuwa ulitwaliwa kutoka humo; wewe u mavumbi na mavumbini utarudi.”
Phonononga Mwanzo 3:19
6
Mwanzo 3:17
Akamwambia Adamu, “Kwa sababu umemsikiliza mke wako na ukala kutoka mti niliokuamuru, ‘Msile tunda lake,’ “Ardhi imelaaniwa kwa sababu yako; kwa kazi ngumu utakula chakula kitokacho humo siku zote za maisha yako.
Phonononga Mwanzo 3:17
7
Mwanzo 3:11
Mungu akamuuliza, “Ni nani aliyekuambia ya kuwa ulikuwa uchi? Je, umekula matunda ya mti niliokuamuru usile?”
Phonononga Mwanzo 3:11
8
Mwanzo 3:24
Baada ya kumfukuzia mbali Adamu, Mungu akaweka makerubi mashariki mwa Bustani ya Edeni, pamoja na upanga wa moto ukimulika kila upande kulinda njia ya kuuendea mti wa uzima.
Phonononga Mwanzo 3:24
9
Mwanzo 3:20
Adamu akamwita mkewe jina Hawa, kwa kuwa atakuwa mama wa wote walio hai.
Phonononga Mwanzo 3:20
Ekuqaleni
IBhayibhile
Izicwangciso
Iividiyo