Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Siku Sita Za Majina Ya MunguMfano

Six Days Of The Names Of God

SIKU 2 YA 6

SIKU 2: ELOHE CHASEDDI – MUNGU WA REHEMA

Maisha siku zote hayatuhakikishii nafasi ya pili. Kuna nyakati ambapo maamuzi yetu mabaya--maneno mabaya kwa rafiki, makosa kazini, maamuzi ya maisha ambayo siyo mazuri--vimetugharimu. Tumepoteza urafiki. Tumefukuzwa kazi. Afya zetu zimeathirika. Hata kama mioyo yetu imebadilika, hakuna uhakika kwamba kila kitu kitakuwa sawa.

Rehema ya Mungu, japo, inatupa nafasi nyingine na nyingine.Elohe Chaseddi—Mungu wa rehema— hutumwagia msamaha na kutuosha na wema wa upendo wake. Siku zote yeye ni wa kweli. Siku zote ni wa rehema. Siku zote mwenye huruma. Tukimpenda na kumuomba msamaha, hutusamehe. Siku zote.

Kwa sababu ni Mungu wa rehema, tunaweza kuishi bila uoga. Siku zote tunaweza kupata amani na moyo ambao huutoa bure kwa wingi. Anatuahidi siku zote kuwa nasi na kutupitisha katika hali zote mbaya. Hata kama makosa tumeyafanya wenyewe, yeye siku zote yuko tayari kutoa msamaha kwa moyo unaotubu.

Badala ya kuhofia kuhusu jana, Mungu anataka tuitazame leo. Tunawezaje kumtumikia leo? Ana mipango gani kwa ajili yetu kuikamilisha leo? Tunawezaje kuwashirikisha wengine Mungu watu leo? Huo ndiyo uzuri wa rehema--nafasi nyingine, tukitazamia mbele, tukitazamia yajayo aliyotuandalia.

siku 1siku 3

Kuhusu Mpango huu

Six Days Of The Names Of God

Kutoka kwenye majina mengi ya Mungu, ametufunulia vipengele vya tabia yake na asili. Zaidi ya Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu, Biblia inaonesha zaidi ya majina 80 tofauti ya Mungu. Hapa kuna majina sita na maana zake kumsaidia mwamini kumkaribia Mungu Mmoja wa Kweli. Dondoo kutoka Experience the Power of God's Names: A Life-Giving Devotional , ya Dr. Tony Evans. Eugene, OR: Harvest House Publishers, 2017.

More

Tunapenda kuwashukuru The Urban Alternative na Tony Evans kwa kutoa mpango huu. Kwa taarifa zaidi, tafadhali https://tonyevans.org/