Siku Sita Za Majina Ya MunguMfano
SIKU 6: EL SIMCHATH GILI – MUNGU FURAHA YANGU ILIYOPITILIZA
Fikiria furaha unayokuwa nayo unapoweza kufanya kitu kwa mara ya kwanza. Yawezekana ulijifunza lugha ngeni ili hatimaye uweze kuwasiliana na wenyeji kwenye nchi nyingine. Au uliweka kilomita na kilomita na mwishowe ulivuka mstari wa mwisho kwenye marathoni. Yawezekana umejaribu miaka mingi ili uweze kuhitimu shahada yako, na mwishowe ulipanda kwenye jukwaaa kuipokea. Unajisikia msisimko wa ajabu, lakini furaha ndiyo hutangulia.
Mambo yote mema hutoka kwa Mungu, na hufurahia katika mambo yote mema. Yeye ndiyo asili pekee ya furaha, na tunapoweka tumaini letu kwake, tunaweza kupata furaha katika mazingira yetu yeyote. Tunaweza kuwa na furaha katikati ya masumbuko yetu yote, kama tumaini letu liko katika Bwana.
Makosa tunayoyafanya ni kutafuta furaha nje ya Mungu. Kama tunajithamini wenyewe kulingana na mawazo ya mtu mwingine juu yetu au mshahara tunaopata au nafasi zetu katika jamii, tunakosa furaha halisi. Tunakosa furaha safarini, furaha ya kugundua, furaha ya moyo uliowazi kwa Mungu. Na tunakosa nafasi adhimu kushiriki furaha hii ya Bwana na wengine. Lakini tunapokuwa tumejawa na furaha inayotoka kwa Mungu, tunaakisi upendo na furaha kwa wale wanaotuzunguka na wanaijua furaha ya kweli.
Kama ibada hii umeiona ya maana, tunataka kukupa zawadi ya kupakua mahubiri kwa jina la Yehovah Yireh. Omba mahubiri kamili ya Tony Evans hapa.
Kuhusu Mpango huu
Kutoka kwenye majina mengi ya Mungu, ametufunulia vipengele vya tabia yake na asili. Zaidi ya Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu, Biblia inaonesha zaidi ya majina 80 tofauti ya Mungu. Hapa kuna majina sita na maana zake kumsaidia mwamini kumkaribia Mungu Mmoja wa Kweli. Dondoo kutoka Experience the Power of God's Names: A Life-Giving Devotional , ya Dr. Tony Evans. Eugene, OR: Harvest House Publishers, 2017.
More