Siku Sita Za Majina Ya MunguMfano
SIKU 4: ESH OKLAH – MOTO ULAO
Umewahi kushuhudia uharibifu uliosababishwa na moto wa msitu? Unakula kila kitu kwenye njia yake, ukivuka kwa haraka kwenye barabara na madaraja na hata kwenye mito. Sasa fikiria moto ulao uliomkubwa kuliko mbingu, na utaweza kuanza kupata ufahamu kidogo wa nguvu ya Mungu.
Lazima tuwe na heshima kwa ajili ya nguvu kubwa na Mungu, lakini pia tunahitaji kukumbuka yeye ni Mungu anayetujali sana. Na kwa sababu hiyo, Ni Mungu anayestahili sifa zetu na ibada wakati wote. Tusimchukulie kirahisi, lakini pia tusiogope kumlilia na kuingia kwenye uhusiano naye.
Ukuu wa Mungu hatuwezi kuuelewa, kama jinsi anavyojihusisha na kila jambo letu dogo la maisha yetu. Ni kwa sababu anatujali sana. Na ndiyo maana tunahitaji kuruhusu moto wake ulao kuunguza mioyoni mwetu.
Yeye ni Esh Oklah, moto ulao, lakini moto uliojaa neema na uvumilivu na huruma. Hutuvuta kwake kwa lengo la sisi kumfanya wa kwanza katika mioyo yetu, akili zetu na nafsi zetu. Na katikati ya huo moto, hujenga upendo mioyoni mwetu.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Kutoka kwenye majina mengi ya Mungu, ametufunulia vipengele vya tabia yake na asili. Zaidi ya Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu, Biblia inaonesha zaidi ya majina 80 tofauti ya Mungu. Hapa kuna majina sita na maana zake kumsaidia mwamini kumkaribia Mungu Mmoja wa Kweli. Dondoo kutoka Experience the Power of God's Names: A Life-Giving Devotional , ya Dr. Tony Evans. Eugene, OR: Harvest House Publishers, 2017.
More