Siku Sita Za Majina Ya MunguMfano
SIKU 5: ELOHE TSADEKI – MUNGU WA HAKI YANGU
Siku zote tunatazamia jambo kubwa linalofuata. Siri ya kuweza kujipanga. Ufunguo wa kujiweka sawa. Mpango halisi wa uthabiti kifedha. Tunasoma vitabu, tunasikiliza podkasti na kujiandikisha kwa ajili ya semina. Wakati mipango, utimamu kimwili na usalama kifedha tunapaswa kuwa navyo, tunahitaji kuwa na uhakika kwamba hatukosi picha halisi wakati tunapotafuta hatua kubwa inayofuata.
Jambo kubwa maishani ni kumfuata Mungu, kufanana naye na maisha yetu kuwa kwa ajili yake. Na kufanana na Mungu maana yake ni kukua katika wema na haki. Kutoka kwa Bwana hushuka rehema, neema, uweza na nguvu--sifa zote hizi tunazihitaji katika maisha yetu na katika ulimwengu wetu. Mungu hutupa vyote tunavyohitaji kupitia kwenye neno lake na Roho ili kuishi maisha tele. Tunapochagua mapenzi yake dhidi ya mapenzi yetu na kujitahidi kufanana na yeye, hutuongoza na kutuelekeza.
Kufuata mapenzi ya Mungu kunaweza kuwa na changamoto kuliko kubaki na hatua sita za kuwa na afya bora au kupunguza vituko nyumbani. Lakini kuna faida zaidi. Tunapomgeukia Mungu na kumpa maisha yetu, hutusamehe na kutuzawadia huruma yake. Hutusaidia kuganga mahusiano yetu yaliyovunjika na kuijaza mioyo yetu haki, neema na amani. Matunda mema hutokana na kumfuata Mungu na kuruhusu haki yake kuongoza hatua zetu.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Kutoka kwenye majina mengi ya Mungu, ametufunulia vipengele vya tabia yake na asili. Zaidi ya Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu, Biblia inaonesha zaidi ya majina 80 tofauti ya Mungu. Hapa kuna majina sita na maana zake kumsaidia mwamini kumkaribia Mungu Mmoja wa Kweli. Dondoo kutoka Experience the Power of God's Names: A Life-Giving Devotional , ya Dr. Tony Evans. Eugene, OR: Harvest House Publishers, 2017.
More