Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Siku Sita Za Majina Ya MunguMfano

Six Days Of The Names Of God

SIKU 3 YA 6

SIKU 3: YEHOVAH YIREH – BWANA ATATOA 

Huna uhakika ni jinsi gani utaweza kulipa bili zako mwezi huu. Hali ya uhusiano wako uko mashakani. Umesikia kutakuwa na kupunguza wafanyakazi kazini kwako, na nafasi yako haina uhakika kwenye kampuni yako. Wakati vitu vya msingi kwenye maisha yako havina uhakika--afya, fedha, makazi, chakula, familia, ajira-- ni kawaida kuogopa, kana kwamba huna kwa kukimbilia. Hapo ndipo unapotakiwa kumwitaYehovah Yireh. Jina hili lililobarikiwa la Mungu linamaanisha “Bwana atatoa,” na ni jina lililoja nguvu na uweza.

Tunapojisikia kuogopa kuhusu ya mbeleni, ni muhimu kumgeukia na kumwita Mungu na kuliitia jina lake. Kila kipawa kilicho chema na kikamilifu kinatoka Kwake, na hakuna ukomo kwa karama na baraka anazotoa. Kumtumaini wakati mwingine inaweza kuwa ndiyo njia pekee ya kutuliza hofu zetu na na kuwa na mawazo chanya.

Linaweza kuwa somo gumu kujifunza, lakini majaribu hapa duniani huimarisha misuri ya imani zetu na kutuleta karibu na Mungu. Kupitia juhudi zetu, hutuonesha dhahiri jinsi anavyotoa hewa kwa ajili ya mapafu yetu kupumua na nuru kwa ajili ya macho yetu kuona. Hutupa kile tunachohitaji ili kuleta ukuaji ndani yetu na wenye faida kubwa sana kwenye ufalme wake. Na siku zote hutoa kwa roho ya upendo.

siku 2siku 4

Kuhusu Mpango huu

Six Days Of The Names Of God

Kutoka kwenye majina mengi ya Mungu, ametufunulia vipengele vya tabia yake na asili. Zaidi ya Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu, Biblia inaonesha zaidi ya majina 80 tofauti ya Mungu. Hapa kuna majina sita na maana zake kumsaidia mwamini kumkaribia Mungu Mmoja wa Kweli. Dondoo kutoka Experience the Power of God's Names: A Life-Giving Devotional , ya Dr. Tony Evans. Eugene, OR: Harvest House Publishers, 2017.

More

Tunapenda kuwashukuru The Urban Alternative na Tony Evans kwa kutoa mpango huu. Kwa taarifa zaidi, tafadhali https://tonyevans.org/