Tafakari Kuhusu HakiMfano
Wakati wa kuwa katika kituo changu kimoja cha huduma, nilifahamishwa kuhusu mwanamke kanisani. Licha ya kusikia mengi kuhusu tabia yake, nilitambua kwamba ufahamu wangu kumhusu ulikuwa wa juu juu. Sikutaka kumbagua, kwa hiyo niliamua kusikiliza hadithi yake. Katika mazungumzo yetu, nilipata uelewa mzuri kuhusu tabia yake na uzoefu uliomfanya awe alivyokuwa wakati huo.
Matukio kama haya ni ya kawaida mno, sio tu katika jamii zetu bali hata katika makanisa yetu. Mara nyingi tunawaona watu wakitengwa kwa sababu ya kuwaelewa kidogo. Labda hata sisi tumehukumiwa isivyo.
Yesu aliweka kiwango cha juu kwa wafuasi wake, akitukumbusha tujizuie kuhukumu na badala yake tukumbatie huruma, neema na uelewa. Hebu kila mara turudi kwenye mafundisho yake kila mara mawazo yetu yanapokuwa yamesongwa na hukumu, na wakati huo hebu sisi kwa uvumilivu tutambue mapungufu yetu wenyewe.
Changamoto:Je, kuna mtu katika jamii yako ambaye unaweza kuchukua hatua za kumfahamu vizuri zaidi? Anzisha mazungumzo naye au mkaribishe mnywe kikombe cha chai au kahawa naye.
Maombi: Bwana, naomba moyo na akili zangu visisongwe na hukumu, na naomba maneno na matendo yangu siku zote yatoe sura ya upendo, neema na uelewa wako.
Kuhusu Mpango huu
Mfululizo wa tafakari ya kila siku kuhusu haki, ulioandikwa na wanawake kutoka kote katika dunia ya Jeshi la Wokovu. Maswala ya haki ya jamii yako mbele sana ya mawazo yetu siku hizi. Mkusanyo huu wa tafakari kuhusu haki ya jamii umeandikwa na wanawake kutoka kote duniani wenye nia na hamu ya kuwasaidia wengine katika jina la Kristo.
More
Tungependa kumshukuru The Salvation Army International kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://salvationarmy.org