Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 10/2024Mfano

Soma Biblia Kila Siku 10/2024

SIKU 31 YA 31

Ahazi akatuma wajumbe kwa Tiglath-pileseri mfalme wa Ashuru, akasema, Mimi ni mtumishi, tena mwana wako; kwea, ukaniokoe mkononi mwa mfalme wa Shamu, na mkononi mwa mfalme wa Israeli, walioniinukia(m.7). Baada ya mfalme wa Ashuru kumsaidia, mfalme Ahazi anakwea aonane naye, na mfalme wa Ashuru anamwambia gharama ya kuwa mtumishi wake na kusaidiwa naye. Inabidi apeleke ramani ya madhabahu mpya kwa Uri, kuhani wa hekalu la Yerusalemu, aijenge. Madhabahu ya BWANA inaondolewa mahali pake ili kuacha nafasi kwa madhabahu hiyo ya mungu mwingine. Ila Ahazi hakutupa kabisa madhabahu ya BWANA, isipokuwa aliiweka pembeni: Mfalme Ahazi akamwamuru Uria kuhani, akisema, Juu ya madhabahu hiyo kubwa uiteketeze sadaka ya kuteketezwa ya asubuhi, na sadaka ya unga ya jioni, na sadaka ya mfalme ya kuteketezwa, na sadaka yake ya unga, pamoja na sadaka ya kuteketezwa ya watu wote wa nchi, na sadaka yao ya unga, na sadaka zao za kinywaji; ukanyunyize juu yake damu yote ya sadaka ya kuteketezwa, na damu yote ya dhabihu; bali madhabahu ya shaba itakuwa kwangu mimi ili niiulizie(m.15). Je, itasaidia kweli kuwa na BWANA hivi pembeni? Vipi na maisha yako, kuna hali ya kufanana?

siku 30

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 10/2024

Soma Biblia Kila Siku 10/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Kumi pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Waebrania, Kutoka na 2 Wafalme. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz