Soma Biblia Kila Siku 10/2024Mfano
Leo tunakutana na wafalme watatu. Menahemu alitawala Israeli kwa miaka kumi akifanya maovu mengi mbele za Mungu. Aliwakosesha Israel wote. Akajipatia kibali cha mfalme wa Ashuru kwa kumhonga fedha zilizochangwa na matajiri wa Israeli.Menahemu akawatoza Israeli fedha hiyo, yaani, wakuu wote wenye mali, kila mtu shekeli hamsini za fedha, ili ampe huyo mfalme wa Ashuru. Basi mfalme wa Ashuru akarejea, wala hakukaa huko katika nchi(m.20). Mwanawe Pekahia alipochukua utawala, akafanya maovu kama baba yake kwa miaka miwili, mpaka jemadari wake Peka alipomwua na kuanza kutawala. Kiongozi ana maana kubwa kwa nchi. Kwa hiyo tuombe kupata na kuchagua viongozi wanyenyekevu wanaomcha Mungu.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 10/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Kumi pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Waebrania, Kutoka na 2 Wafalme. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz